Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema nchi yake haitishwi na hatua
iliyochukuliwa na serikali ya Marekani, kusitisha msaada wake wa kijeshi kwa
nchi hiyo, kwa kile inachodai Rwanda inawafadhili waasi wa M23 wanaopigana na
serikali mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.
Rais Kagame amesema anashangazwa na hatua ya
Marekani kuihukumu nchi hiyo kwa makosa ambayo Rwanda haihusiki kwa lolote wala
haifadhili kundi lolote la waasi nchini DRC na kuongeza kuwa kufanya hivyo ni
kutoitendea haki Rwanda. Rais Kagame amesema kamwe Rwanda haijawahi
kuhusisha watoto wadogo kwenye jeshi lake wala kuunga mkono kutumikishwa kwa
watoto wadogo kama wanajeshi kwenye kundi la M23.
Serikali ya Marekani ilitangaza majuma kadhaa
yaliopita kusitisha msaada wake wa kijeshi kwa serikali ya Rais Kagame kufuatia
hatuwa hiyo inayotajwa ya kuwafadhili waasi wa kundi la M23 wanaopambana na
serikali ya Rais Joseph Kabila.
No comments:
Post a Comment