EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, October 18, 2013

BUNGE LA CONGRES NA WAPINZANI WAPITISHA MUSWAADA WA TILIONI 16



Wabunge wa bunge la Congress na lile la wawakilishi, wamepitisha muswada wa sheria utakaoruhusu kupatikana kwa fedha zinazofikia kiasi cha trilioni 16, fedha ambazo sasa zinawezesha kufunguliwa kwa shughuli za serikali hadi mwezi January mwaka 2014.
Raisi Barack Obama wa Marekani

Hapo jana wabunge wa Congress walipitisha kwa kishindo mapendekezo ya chama cha Democrats na yale ya Republican na mapema hii leo asubuhi, bunge la Seneti na lenyewe likapigia kura muswada huo ambao wabunge 256 waliunga mkono.







Muswada huo sasa unatarajiwa kuwasilishwa kwa rais Barack Obama ambaye amesema atautia saini mara moja, ili kuona shughuli za serikali zikianza haraka baada ya kuwa zimesimama kwa muda kutokana na kukosekana kwa fedha.
Kupitishwa kwa muswada huo kunatoa nafasi ya kufunguliwa kwa ofisi za serikali na kujiendesha hadi January 15 mwaka 2014 jambo ambalo hatahivyo linaonekana kuwa bado halijatatua tatizo.
Katika hatua nyingine rais Barack Obama amewapongeza wabunge wa Republicans na wale wa chama chake kwa kufikia makubaliano ili kuruhusu Serikali kujiendesha.


No comments:

Post a Comment