EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, October 28, 2016

MBAO FC YAWATISHA YANGA WASEMA WAO SI WAMCHEZOMCHEZO

Wakati Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ikiendelea leo Ijumaa Oktoba 28, 2016 kwa mchezo mmoja, kwa siku ya kesho Jumamosi Oktoba 29, mwaka huu kutakuwa na michezo mitano wakati kwa siku ya Jumapili kutakuwa na michezo miwili ya raundi ya 13, ligi ikielekea ukiongoni mwa mzunguko wa kwanza.

kesho itakuwa ni zamu ya Toto Africans ya Mwanza dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa CCM Kirumba na Mbeya City ya Mbeya itakayokuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

KAULI YA FERGUSON JUU YA UBINGWA EPL 2016/2017 YAWATIA WAZIMU PEP, NA MOURINHO

MENEJA LEKENDARI Sir Alex Ferguson anadhani Manchester City ndio wenye nafasi kubwa kutwaa Ubingwa wa England Msimu huu huku akiwa kimya kuhusu nafasi ya Kikosi cha Chelsea chini ya Meneja wao Antonio Conte.
Sir Alex Ferguson, mwenye Miaka 74, aliongea hayo akiwa huko Nurenberg, Germany alikokwenda kupokea Tuzo ya Walther Bensemann ambayo hutunukiwa Watu waliotoa Utumisha Uliotukuka kwenye Soka.
Tuzo hiyo hutolewa kwa ajili ya Kumbukumbu ya Bensemann ambae ndie anasemekana ni Muasisi wa Soka la Germany ambae alianzisha Jarida la Michezo, Kicker, Mwaka 1920.

HENDERSON WA LIVERPOOL NDIYE MCHEZAJI ALIYETEMBEA ZAIDI MSIMU HUU

JORDAN HENDERSON
Mtandao wa kimataifa wa LFC  umeripoti muda mfupi uliopita kuwa tafiti zinaonyesha kwamba kiungo wa kati wa klabu ya Liverpool Jordan Henderson ndiye mchezaji aliyeongoza kutembea umbali mrefu zaidi akiwa uwanjani kwenye ligi kuu uingereza msimu huu kuliko mchezaji yeyote anayeichezea ligi hiyo maarufu duniani.
kwa mujibu wa mtandao huo ni kwamba Henderson ametembea  (106.49km)

MOURINHO, MOYES KWA ‘PILATO’ WA FA!

KOCHA WA MANCHESTER UTD JOSE MOURINHO
MAMENEJA wa Manchester United Jose Mourinho na David Moyes wa Sunderland wamefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kwa makosa mbalimbali.
MOURINHO
Mourinho ameshitakiwa kutokana na matamshi yake juu ya Refa Anthony Taylor ambae Wiki iliyopita alichezesha pambano la Liverpool na Man United huko Anfield na kwisha 0-0.
Uamuzi huo wa FA umekuja baada ya Chama hicho kuona amevunja Sheria kwa kuongea kuhusu Marefa kabla ya Mechi wanayopangiwa.
Mara baada ya Refa Taylor, mwenye Miaka 37 na anaetoka Kitongoji cha Wythenshawe kilichopo Maili 6 tu toka Old Trafford Nyumbani kwa Man United huko Jijini Manchester, kuteuliwa kuliibuka malalamiko, na hasa Mashabiki wa Liverpool, ambao walilivalia njuga kwenye Mitandao ya Kijamii.