Uongozi Wa Wilaya Ya Mtwara Unakabiriwa Na Changamoto Ya
Kutokuwa Na Chanjo Ya Mbwa Katika Hospitali Zake Hali Iliyotajwa Kuwa Ni Tatizo
Kubwa Kwa Wakazi Wa Wilaya Hii Hasa Mara Baada Ya Kutokea Kwa Mlipiko Wa Mbwa
Wengi Wasio Na Matunzo Maalum Katika Mitaa Mbalimbali Hususani Katika Maeneo Ya Mtwara Manispaa.
Hayo Yamebainika Mara Baada Ya Kipindi Cha Amka Na Pride
Kupitia Kipengere Chake Cha Chimbuachimbua Kutembelea Katika Mtaa Wa Majengo
Kata Ya Chuno Mapema Leo Asubuhi Na Kukutana Na Wakazi Wa Mtaa Huo Ambao Walielezea
Namna Wanavyosumbuliwa Na Ongezeko Hilo La Mbwa Ambao Wamekuwa Ni Kero Na
Tishio La Amani Ya Wakazi Wa Mtaa Huo
Hasa Kwa Watoto Wadogo.
Katika Maelezo Yao Wananchi Hao Walisema Mpaka Kufikia Hivi
Sasa Idadi Ya Mbwa Ambao Wamekosa Mahali Maalum Pa Kutunza Imezidi Kuongezeka
Na Mtaa Umekuwa Na Kero Kwani Mbwa Hao Wamekua Waharibifu Wa Mifugo Kama Vile
Kuku Na Bata Pamoja Na Kuwadhuru Watoto Na Kuharibu Bustani Za Mboga Kwa
Kufanya Ni Sehem Za Kujilaza Wakati Wote.
Akieleza Kwa Masikitiko Makubwa Moja Kati Ya Wakazi Wa Mtaa
Huo BI: Zainabu Said Mputeni Alisema Yeye Ni Muathiriwa Wa Kwanza Wa Mbwa Hao
Kwani Mjukuu Wake Aitwaye Shedrak Makame Umri Ni Miaka Nane Ameng’atwa Na Mbwa
Na Kukosa Matibabu Huku Nakiorodhesha Vituo Vya Afya Kama Vile Cha Mahurunga,Nanguruwe
Na Hospitali Ya Mkoa Ya Ligula Ambako Alimpeleka Motto Huyo Na Kukosa Msaada Kwakua
Hakuna Chanjo Ya Mbwa.
BI: Zainabu Alisema Kuwa Serikali Ni Lazima Ijipange Na Kulichukulia Suala Hili Kuwa Ni La Lazima Kwa Kuweka Dawa Ama Chanjo Za Mbwa Ili Kuepusha Usmbufu Kama Alioupata ,Kwa Upande Wake Mwenyekiti Wa Mtaa Huo Ndg Mwangaza Alikiri Kuwepo Kwa Usumbufu Huo Utokanao Na Mbwa Na Kusema Kuwa Wanaiomba Serikali Kuwasaidia Kutokomeza Mbwa Hao Hata Kwa Kuwaua Ili Kuepusha Madhara Wayapatayo Sasa.maelezo ya wananchi wengine walioko katika eneo hilo walielezea mbwa hao kujaaa katika eneo la machinjio ya nyama yaliyoko mtaani hapo ambayo ndiyo yanayogawa nyama ndani ya mji wa mtwara na kusema kuwa mbwa hao wamekuwa wakishinda katika maeneo hayo ya machinjio na kuiba nyama wakati mwingine pindi shughuri za uchinjaji zinapomalizika mbwa hao upita kulambalamba na kulala juu ya maeneo ya kulaza nyama hali ambayo kiafya si nzuri kwani siku ya pili nyama nyingine huwekwa maeneo hayohayo bila kusafishwa na kusema kuwa inaweza kuleta hatari ya mlipuko wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi na watumiaji wa nyama kwa ujumla, lakini wananchi hao walifika mbali na kuitaka serikali kusimamia sheria ya mbwa na kwamba asiye na fensi au banda maalum nyumbani kwake asipewe ruhusa ya kufuga mbwa kwani hiyo ndiyo sababu ya mbwa wengi kuzagaa mitaani hovyo kwakua hawana makazi maalum.
No comments:
Post a Comment