Siku chache baada ya nchi za Afrika, kutishia kujiondoa kwenye mkataba wa Roma uliounda Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema nchi hizo, zina dhima ya kutimiza wajibu wao wa kimataifa na kushirikiana kikamilifu na mahakama hiyo yenye makao yake mjini Hague, Uholanzi.
![]() |
Katibu mkuu UN Ban Ki Moon |
Ban Ki moon amesema Umoja wa Mataifa unachunguza kwa makini mapendekezo yaliyotolewa na Umoja wa Afrika wikendi iliyopita, lakini akasisitiza kuwa, Nchi za Afrika zinapaswa kuendelea kutoa ushirikiano usio wa masharti kwa ICC. Matamshi ya Ban yanaashiria uwezekano wa UN kutokubali pendekezo la AU, ambalo pamoja na mambo mengine linataka kesi za Rais wa Kenya na Naibu wake mbele ya ICC zisimamishwe kwa mwaka mmoja.
Huku hayo yakijiri, Mahakama kuu nchini Kenya imetupilia mbali kesi iliyokuwa imewasilishwa kutaka Rais Uhuru Kenyatta kuzuiwa kwenda mjini The Hague kujibu mashtaka yanayomkabili mbele ya ICC.
No comments:
Post a Comment