Capt. John Kivunge, a Tanzanian Staff Officer with JOC, reads a program of the brief ceremony. Prayers from a chaplain.Prayers from an Imam for the fallen peacekeepers. Military salute as the 'Last Post' rings out by Nigbatt in honour of the fallen heroes. Start of the last journey home. ...
AUNT EZEKIEL AMTOSA MUMEWE
Wengi walitegemea kuwa Aunt Ezekiel ataungana na mumewe Sunday katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani lakini hali imekuwa ni tofauti.... Aunt anayetumia jina la Rahma baada ya kubadili dini ili aolewe na mwanaume huyo, amemtosa mkaka huyo na kuendelea kula bata nchini huku akidai kuwa mumewe hana mengi. "Sina mpango wowote wa kuondoka nchini ...
DRC NI UWANJA WA VITA KATI YA TANZANIA NA RWANDA ( PROX WAR)
PROX WAR au Proxy Warfare ni vita inayopiganwa kwa kupitia sehemu nyingine. Katika vita 'ya kawaida' mapigano huwa kati ya nchi na nchi.Kwa mfano, Vita ya Kagera ilkuwa kati ya Tanzania na Uganda, na mapambano yalitokea katika nch zote mbili. Katika proxy war hali ni tofauti. Nchi A inaweza kupigana vita na nchi B katika nchi C.Yaani kwa ufasaha zaidi, kwa mfano, kuna mapambano katika nchi C kati ya jeshi la nchi hiyo na waasi, kisha nchi A inapeleka askari wake kuilisaidia jeshi la serikali la nchi C, na nchi B inapeleka askari wake (au inasaidia kwa siri) kusaidia waasi wanaopigana na serikali ya nchi C. Naomba...
HATIMAYE LUDOVICK JOSEPH NAYE AACHIWA KWA DHAMANA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia kwa dhamana Ludovick Joseph
anayeshitakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema
Wilfred Lwakatare, baada ya kusota rumande kwa zaidi ya miezi minne.Ludovick
aliachiwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana baada ya kutimiza
masharti ya dhamana yaliyotolewa Juni 10 mwaka huu.Washitakiwa
hao waliofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Machi 18 mwaka huu,
wanakabiliwa na shitaka la kutaka kumdhuru Mhariri wa gazeti la
Mwananchi, Dennis Msacky kwa kutumia sumu....
DALADALA YANUSURIKA KUINGIA BUCHANI MWENGE
Daladala lenye namba za usajili T 741 AEG baada ya kuhama njia na kuparamia mtaro uliopo jirani na bucha eneo la Mwenge. Daladala lenye namba za usajili T 741 AEG linalofanya safari zake kati ya Temeke na Mwenge asubuhi hii nusura liingie katika bucha iliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar katika barabara iendayo Afrika Sana. Daladala hilo lilisaidiwa na mtaro uliopo mbele ya bucha hiyo baada ya dereva wake kushindwa kuliongoza na kuhama barabara. Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio, daladala hilo halikuwa na abiria na hakuna mtu aliyejeruhiw...
WANAJESHI WENGINE WATATU WA TANZANIA WAFARIKI DUNIA HUKO SUDANI, MAPIGANO MAKALI YAIBUKA HUKO KONGO KATI YA SERIKALI NA WAASI WA M23
WINGU zito limetanda kwa askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), katika nchi za Sudani Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Wakati Watanzania wakiendelea kuomboleza vifo vya wanajeshi saba wa jeshi hilo waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, Sudani kwa kushambuliwa na waasi, nchini DRC yamezuka mapigano makali baina ya waasi na majeshi ya Serikali. Mapigano hayo yameripotiwa kuibuka kati ya Wanajeshi wa Serikali na waasi karibu na mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).Msemaji wa wapiganaji wa waasi wa M23, ameliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza...
MBOWE ATIWA MBARONI NA KUHOJIWA KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Freeman Mbowe, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kutoa kauli
za uchochezi dhidi ya jeshi hilo, vyombo vya dola na serikali kwa
ujumla.
Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa na Msemaji wake, Mrakibu Mwandamizi,
Advera Senso, imesema kuwa Mbowe amekuwa akitoa kauli ambazo zimekuwa
na mlengo wa uchochezi na kuijengea jamii taswira hasi juu ya vyombo vya
ulinzi na usalama na kuwafanya wananchi kuwa na hofu.
Mbowe akiandamana na mawakili, Nyaronyo Kicheere na Peter Kibatara,
alijisalimisha mwenyewe makao makuu ya polisi majira ya saa 8:30 mchana,
mara tu baada...
No comments:
Post a Comment