EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, October 18, 2013

RAISI IAN WA BOTSWANA AITAKAN JUMUIYA YA KIMATAIFA KUSHIRIKIANA KUPAMBANA NA UJANGIRI



Rais Ian Khama wa Botswana amesema kuwa kutokana na kuenea kwa ujangili na biashara haramu ya wanyama pori na bidhaa husika, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuimarisha ushirikiano, na kuchukua hatua zenye ufanisi zaidi za kulinda wanyama pori. 
 
Raisi Ian Khama wa Botswana

Ametoa kauli hiyo wakati alipohudhuria mkutano maalum wa tano wa mawaziri kuhusu mazingira ya Afrika, ambapo Rais Khama amesema hivi sasa biashara haramu ya wanyama pori na bidhaa zinazotengenezwa kutokana na wanyama hao zimekuwa nyingi, na mwelekeo huo utatishia mafanikio ya muda mrefu ya kuwalinda wanyama pori.




Amesema kuwa Afrika inahitaji uungaji mkono wa dunia katika kutatua suala la biashara haramu ya wanyama pori, kwani ni mahitaji ya bidhaa zinazotengenezwa kutokana na wanyama hao, yanayosababisha ujangili barani Afrika, na kutishia maisha ya baadhi ya wanyama pori.
Rais Khama pia amesema, mwezi Desemba mwaka huu, serikali ya Botswana itashirikiana na jumuiya ya kimataifa ya uhifadhi wa mazingira ya asili, kuandaa mkutano wa ngazi ya juu wa kuwalinda ndovu wa Afrika, ili kutoa wito wa kuitaka dunia ichukue hatua kuzuia biashara haramu za meno ya ndovu.


No comments:

Post a Comment