Ivory Coast na Burundi zimefikia makubaliano ya
kuimarisha ushirikiano wa kiusalama kati yao.
![]() |
raia wa nch ya Ivory Coast wakiwa wamebeba bendera ya nci yao |
Waziri wa Usalama wa Jamii wa Burundi amesema akiwa
mjini Abidjan nchini Ivory Coast kuwa Burundi na Ivory Coast zimeazimia
kuboresha ushirikiano wa kiusalama kati yao. Akiwa ziarani nchini Ivory Coast, Waziri wa Usalama
wa Jamii wa Burundi amepata fursa ya kukitembelea kikosi cha polisi wa Burundi
walioko nchini Ivory Coast, katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa
Mataifa. Laurent Kavakure, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi
Februari 21 mwaka huu, alifanya ziara nchini Ivory Coast ambapo katika
mazungumzo yake na viongozi wa nchi hiyo, walijadili suala la ushirikiano
katika masuala ya usalama kati ya nchi hizo mbili.
No comments:
Post a Comment