EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, March 1, 2014

NDANDA YAENDELEZA UBABE NYMBANI TESEMA WAKUBALI KICHAPO CHA BAO MOJA KWA NUNGE

KOCHA MKUU NDANDA FC..DENIS KITAMBI (TISHETI YA BLUE)
Timu ya ndanda ya mkoa wa mtwara inayoshiriki ligi daraja la kwanza leo imeendelea kujipa tumaini la kuvuka daraja na kuingia ligi kuu baada ya kuilaza timu ya tesema toka dar es salaam katika mcezo uliopigwa ndani ya dimba la nangwanda mkoani mtwara jioni ya leo
WACHEZAJI NA WAAMUZI WAKITOKA UWANJANI BAADA YA MPIRA KUMALIZIKA
ambapo mtanange huo ulianza majira ya saa kumi kamili za jioni na katika kipindi cha kwanza hali ya mchezo ikiwa ya vuta ni kuvute na kupelekea mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika hakuna timu iliyoona lango la mwenzake,
WACHEZAJI WA NDANDA WAKICHOJOA VIATU BAADA YA MCHEZO
lakini waliporejea tena dimbani katika round ya pili ya kipindi cha lala salama mchezo ulionekana kubadilika na kuwa wa kasi zaidi huku ndanda wakikosa nafasi nyingi za wazi kwa kupiga mipira nje na baada dk ya 63 mchezaji Salum Mineli wa ndanda Fc aliweza kuiandikia timu yake bao pekee na  la ushindi lililodumu mpaka mwisho wa mchezo huo,

ndanda sasa kwa mijibu wa kocha wao Denis Kitambi jumamosi ijayo watacheza na timu ya Green Warrious toka dar se salaam hapahapa mkoani mtwara ikiwa ni mechi yao ya mwisho kucheza nymbani katika zile tatu ambapo mechi ya kwanza waliweza kuifunga Afrikan LYION bao moja kwa nunge jumamosi iliyopita ya february 22.
NDANDA HAOOOOO
ambapo kocha wao ameieleza swacotz forum mara baada ya mchezo huo kuwa wao wamejipanga vya kutosha na kwamba mgeni wao atarajie kufungwa na si ushindi kwakua ameshaona wenzake jinsi walivyohangaishwa.
NDANDA WAKIFURAHIA USHINDI

No comments:

Post a Comment