EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, February 11, 2014

barabara ya Dar--arusha yasombwa na mvua

Mvua yakata barabara Dar - Arusha


MVUA kubwa zilizonyesha usiku wa kuamkia jana mkoani Kilimanjaro, zimekata mawasiliano ya barabara kuu ya Dar es Salaam-Arusha na kusababisha magari kukwama kwa saa nane Hedaru wilayani hapa.
Taarifa zilizopatikana jana na kuthibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Same, Shaibu Ndemanga, zilieleza kuwa mvua hizo zilisababisha mafuriko yaliyobomoa makalavati mawili ya barabara hiyo.
Kutokana na hali hiyo zaidi ya magari 400 yalikwama eneo hilo, ambapo wasafiri kutoka mikoa mbalimbali walishindwa kuendelea na safari kuanzia alfajiri mpaka saa tatu asubuhi jana waliporuhusiwa kuendelea na safari.
“Tumefanikiwa kutengeneza barabara nyingine ya mchepuko kwa kuweka makalavati ya dharura na
leo (jana) kuanzia saa tatu asubuhi magari hayo yalianza safari kwenda mikoa mbalimbali na nchi jirani baada ya Serikali kufanya juhudi za makusudi kumaliza tatizo hilo. “Tayari Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Maafa, Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoani hapa, walimwagiza Mkandarasi anayetengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha lami, kuweka upya makalavati ya dharura ili kutatua tatizo hilo,” alisema.
Barabara hiyo kwa sasa iko katika ujenzi wa kiwango cha lami kati ya Mombo na Same chini ya Kampuni ya ujenzi ya kimataifa ya Dott Service Limited.
Hadi jana hakukuwa na taarifa za wananchi wa maeneo hayo kupoteza maisha au kukosa makazi, ingawa Mkuu wa Wilaya aliahidi kutoa taarifa kamili ya uharibifu wa mali kesho.
Mmoja wa abiria aliyekuwa akisafiri kwa basi la Lim Safari kutoka Arusha kwenda Dar es Salaam, Ngilenengo Urasa, alishauri kampuni hiyo ya ujenzi kufanya uhakiki wa mara kwa mara katika michepuko ya barabara kuhakikisha hakuna madhara yanayoweza kutokea na kusababisha kukwama kwa abiria na magari ya mizigo.
SOURCA: Habari leo

No comments:

Post a Comment