EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, October 9, 2013

KOFI ANNAN: AFRIKA YAJITIA AIBU KUJIONDOA ICC



                                          JOHHANESBURG.
Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amezikosoa vikali nchi za Afrika, zinazotishia kujiondoa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) akisema kuwa hiyo ni alama ya aibu na fedheha kwa Afrika.
kofi anan-katibu mkuu mstaafu UN

Annan, ameyasema hayo katika sherehe ya kumuenzi Askofu Desmond Tutu, aliyekuwa miongoni mwa viongozi wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka ya 1984.
Annan amesema kama Waafrika wangeweza kutendewa uadilifu katika nchi zao, kusingekuwepo haja ya kwenda kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.
Amesema kuwa katika bara la Afrika ambalo limeshuhudia migogoro iliyosababisha umwagikaji wa damu, ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na hata mauaji ya kimbari, inashangaza kusikia watu wanasema kuwa kutafuta haki katika mahakama ya ICC kutakwamisha juhudi za kurejesha amani.
kofi anan-katibu mkuu mstaafu UN

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) inakosolewa na Waafrika kwamba inawalenga viongozi wa bara hilo pekee, na kufumbia jicho jinai zinazofanywa na viongozi wa nchi za Magharibi katika nchi mbalimbali duniani.

No comments:

Post a Comment