NA: MATHIAS KANAL........IRINGA
Mapema hii leo askari Pacificus Cleophace Simon mwenye No G.2573 mtuhumiwa
wa kesi ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha channel ten mkoani Iringa
Daud Mwangosi amefikishwa mahakamani kusomewa shitaka la kesi hiyo kwa mara ya
kwanza
Cleophace amesomewa shitaka hilo linalomkabili kutokana na mauaji ya
mwandishi huyo wa habari yaliyotokea kijiji cha Nyololo Wilayani Mufindi Mkoa
wa Iringa wakati wa mkutanao mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema
uliotarajiwa kufanyika septemba 2, 2012 na kuhutubiwa na katibu mkuu wa chama
hicho Dkt Wilbroad Slaa
Hata hivyo serikali iliikiandikia barua
chama cha demokrasia na maendeleo chadema ya kuwataka kusitisha mkutano
kwa siku hiyo kwa sababu siku hiyo hiyo sensa ya watu na makazi ilianza na
badala yake ilikitaka chama hicho kusubiri hadi sensa itakapomalizika septemba
8, 2012
Chama cha chama cha demokrasia na maendeleo chadema hakikubaliana na
maagizo hayo ya serikali kwa kuwa tayari kilikuwa na barua ya kuruhusiwa
kufanya mkutano huo hivyo kupelekea kuwa na mvutano kati ya jeshi la polisi na
wafuwasi wa chama hicho hivyo kupelekea polisi kupiga mabomu ya machozi kwa
ajili ya kuwatawanya wafuasi hao waliojitokeza kwenye mkutano huo.
Baada ya uchunguzi wa chanzo cha kifo hicho mkemia mkuu alitoa uthibitisho
kuwa kilichomuua Mwangosi ilikuwa ni kemikali aaina ya NItrate na Cloride
zilizokutwa zimebakia katika mwili wa Marehemu Mwangosi.
Wakati huo huo kesi ikiwa inaendelea mapema hii leo, askari wa jeshi la
polisi alevaa nguo za kiraia jina halijafahamika simu yake iliita mahakamani na
kutoka nje kwa ajili ya kuipokea kitendo ambacho ni kinyume na utaratibu wa
uendeshaji wa mahakama lakini hakuchukuliwa hatua yoyote.
Sambamba na hayo Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa
Bw Frank Leonard ambaye ni mwandishi wa gazeti la habari leo na mmiliki wa
TOVUTI ya BONGO LEANKS alikamatwa na askari na kutolewa nje ya mahakama kwa
kuwa alishika simu wakati mahakama inaendelea hivyo kuhisiwa alikuwa anapiga
picha.
Leonard alifikishwa kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo
huku waandishi wote walihudhuuria mahakamani hapo wakiwa nje ya kituo hicho
kusubiri hatma ya kesi hiyo.
Haikuchukua hata dakika 2 Leonard akaachiwa huru kwa kuwa jeshi la polisi
liijichukulia sheria mkononi wakati jambo lolote la kimahakama linapaswa
kuamuliwa na kjaji anayeendesha kesi hiyo.
Aidha jaji mfawidhi wa mahakama ya Iringa Bi Mary Shangai ameahirisha kesi
hiyo hadi msajilin wa mahakama atakapoitisha kikao cha kupanga lini kesi hiyo
isikilizwe.
SIKILIZA HAPA ILIVYOKUWA................
No comments:
Post a Comment