EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, February 13, 2014

WENGER & MOYES WAAMINI KATIKA SARE TU!!!!!!!!!!!



WENGER_N_MOYESBAADA ya Sare ya 0-0 huko Emirates kati ya Arsenal na Manchester United, Mameneja wa Timu hizo, Arsene Wenger na David Moyes, wamezungumzia Mechi hiyo.
DAVID MOYES:
-“Ninachoweza kusema ni kuwa tutajaribu kushinda Gemu yetu ijayo! Kama ipo Klabu ambayo ni wazuri kushinda Gemu Kipindi cha Pili cha Ligi ni Man United.”
-”Bado Wachezaji wana ari ya ushindi licha ya kutwaa Mataji mengi. Mmemuona Vidic alivyo mzuri, Rio alikuwa safi alipoingia. Wote washawahi kuwa Washindi.”
-Akiongelea Robin van Persie kukosa Bao ambalo lingewapa ushindi: “Lile lingekua Bao safi baada muvu nzuri ya Rooney lakini Kipa aliokoa!”
ARSENE WENGER:
-“Ilikuwa muhimu tusifungwe! Lakini ilikuwa muhimu tushinde! Nadhani tulikuwa na mchecheto!”
-“Tulitilia mkazo sana Gemu hii pengine hilo lilituzuia kwenda mbele kushambulia kwa sababu ya zile Goli 5 tulizofungwa Jumamosi!”
+++++++++++++++++++++++
NINI KIJACHO:
Wakati Arsenal wataikaribisha Liverpool Uwanjani Emirates Jumapili kwenye Mechi ya Raundi ya Tano ya FA CUP, Man United wao hawana Mechi hadi Februari 22 watakapoenda Ugenini kucheza na Crystal Palace kwenye Mechi ya Ligi Kuu England, na mwanya huu wa Siku 10 umewapa nafasi kwenda huko Dubai, Falme za Nchi za Kiarabu, kupiga Kambi ya Mazoezi ya eneo lenye unafuu kidogo wa hali ya hewa ya Joto.
MATOKEO:
Jumatano Februari 12
Arsenal 0 Man United 0
Everton v Crystal Palace [IMEAHIRISHWA]
Man City v Sunderland [IMEAHIRISHWA]
Newcastle 0 Tottenham 4
Stoke 1 Swansea 1
Fulham 2 Liverpool 3
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Chelsea 26 17 6 3 48 21 27 57
2 Arsenal 26 17 5 4 48 26 22 56
3 Man City 25 17 3 5 68 27 41 54
4 Liverpool 26 16 5 5 66 32 34 53
5 Tottenham 26 15 5 6 36 32 4 50
6 Everton 25 12 9 4 37 26 11 45
7 Man United 26 12 6 8 41 31 10 42
8 Southampton 25 10 9 7 37 29 8 39
9 Newcastle 26 11 4 11 32 38 -6 37
10 Swansea City 26 7 7 12 33 36 -3 28
11 West Ham 26 7 7 12 28 33 -5 28
12 Aston Villa 26 7 7 12 27 36 -9 28
13 Hull 26 7 6 13 25 31 -6 27
14 Stoke 26 6 9 11 27 41 -14 27
15 Crystal Palace 25 8 2 15 18 34 -16 26
16 Norwich 26 6 7 13 19 39 -20 25
17 West Brom 26 4 12 10 30 38 -8 24
18 Sunderland 25 6 6 13 25 38 -13 24
19 Cardiff 26 5 7 14 19 44 -25 22
20 Fulham 25 6 2 18 26 58 -32 20
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi Februari 22
1545 Chelsea v Everton
1800 Arsenal v Sunderland
1800 Cardiff v Hull
1800 Man City v Stoke
1800 West Brom v Fulham
1800 West Ham v Southampton
2030 Crystal Palace v Man United
Jumapili Februari 23
1630 Liverpool v Swansea
1630 Newcastle v Aston Villa
1900 Norwich v Tottenham

No comments:

Post a Comment