NA MSHAMU NGOJWIKE
KUFUATIA
hali ya hewa ya mvua ya Beira, wachezaji wa Azam Fc wapatiwa vifaa hususani
viatu maalum vya kuchezea katika sehemu yenye unyevunyevu.
Azam iko nchini
msumbuji leo watashuka dimbani tayari kwa pambanao la marudiano dhidi ya
wenyeji Ferroviario da Beira litalokafanyika kwenye uwanja wa wenyeji hao saa 9
alasiri za Msumbiji (saa 10 za Tanzania).
Wawakilishi
hao wa Tanzania wanahitaji ushindi au sare kutokana na ushindi wa 1-0 katika
mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Azam fc wakiendelea na mazoezi nchini Msumbiji,katika uwanja wa Beira.
Akizungumza
na SWACOTZ FORUM kwa mtandoa, Katibu Mkuu wa Azam, Nassor Idrissa, alisema kuwa hali kama hiyo
iliwahi kuwatokea miaka ya nyuma katika maandalizi ya ligi Tanzania bara,wakiwa
na uhakika hali hiyo kutoathiri matokeo mabaya ya mechi.
"Tulishakumbana
na hali kama hii wakati fulani nchini Uganda wakati tuanajitayarisha na ligi,
mazingira yalikuwa magumu sana na tulijikuta tunapigwa na Bunamwaya maboa 4-0, kabla
ya mapumziko, kutokana na wachezaji kuteleza ovyo lakini baada ya kubadili
viatu tulifanikiwa kurejesha magoli yote na tukapata sare ya 4-4, tokea hapo
tumekuwa na tahadhari kubwa ya mambo haya"alisema.
Mshambuliaji kipre Tche tche kulia akiwa na Keita Raia wa cameroon
Nassor alisema
kulinagana na taarifa zilizokuwa
zimepatikana mapema uongozi ulikuwa na dondoo za hali ya hewa ya Beira na hivyo
matayarisho muhimu yalifanyika kwa upande wa vifaa hususan uwepo wa viatu
maalum vya kuchezea katika sehemu yenye unyevunyevu ili kuhimili utelezi na
hatimaye kupata matokeo yanayohitajika.
Katika Mchezo
wa Jumapili umepangwa kuchezeshwa na waamuzi kutoka Zambia, Azam Azam itafaulu kusonga mbele itakabiliana na
timu ya Shirika la Umeme la Zambia, Zesco kati ya Machi 1 na 2 jijini Dar es
Salaam na kurudiana juma moja baadaye mjini Ndola.
No comments:
Post a Comment