EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, February 15, 2014

Wimbo mpya wa Mb Dogg ni balaa



NA MSHAMU NGOJWIKE, DAR 

WIMBO mpya unaokwenda kwa jina la ‘Baby Mbona Umenuna’ wa mwimbaji Mbwana Mohamed maarufu kama Mb Dogg utakuwa moto wa kuotea mbali, utakapomalizika kurekodiwa katika Studio za Maccopa.

Mb Dogg ndani ya pozi
Akizungumza na SWACOTZ FORUM, Mkurugenzi wa Kampuni ya Qs Mhonda J Entertainment, Joseph Mhonda, alisema wimbo huo ambao unaelekea kukamilika utamuweka juu msanii huyo kutokana na jinsi alivyouandaa


Alisema kwamba Mb Dogg ni msanii aliyejichimbia kwa muda mrefu akiwa na mahitaji ya kurudi kwenye nafasi ya juu kama awali, jambo lililomfanya atulie na kufanya kazi ya uhakika.

“Qs inafanya juhudi kubwa kuleta ile ladha halisi ya msanii huyu aliyetingisha katika anga za muziki wa Bongo Fleva, enzi hizo akitokea Tip Top ‘Connection’.

Mb Dogg anatokea katika kampuni hiyo kwa sasa, akiwa sambamba na Nay wa Mitego anayetamba na wimbo wa Muziki Gani, aliyeimba kwa kushirikiana na Diamond.

No comments:

Post a Comment