EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, August 20, 2014

Gobole mtunzi wa mnanda anayeambulia 500,500 za maji!!!!!


Na mshamu ngojwike

KWA wapenzi wanaoufatilia kwa undani mziki wa asili wa mnanda hapana shaka kushindwa kumfahamu nguli wa mashairi ya mnanda,Hamza Hamisi 'Gobole'.


Maadhi yake yote ya mziki wa mnanda ni asili ukianzia kwenye ala za mziki mwenye. Kama unavyojuwa mnanda hutumia ngoma,visoda,malimba na vitu vingine vya asili,ili kunogesha mziki huu.

Mnanda ndio mziki wetu wa asili ya kitanzania na ndo maana marehemu Omari Omari alikubalika Africa kusini alipoenda kufanya shoo Johannesburg kwa kuimba nyimbo za asili yetu,ambayo ni mnanda.



 Enzi za uhai wake mfalme huyu wa mnanda marehemu Juma Juma 'Lupozi' aliwahi kusema kuwa anakipaji çha kuzaliwa nacho.Marehemu lupozi alimuamini gobole katika utungaji wa nyimbo zake baada ya kuona kazi alizofanya na omari omari.


Gobole alizaliwa 1976 jijini Dar es salaam na kupata elimu yake ya msingi kwenye shule ya msingi Dundani iliyopo mkuranga,na kujiunga na sekondari mînaki kisawe mkoani pwani.

Unaweza ukasema maisha ya Gobole ni ya kisanaa toka akiwa shule ya msingi alipokuwa anatunga mashairi ya darasa na shule.

Kwa muda wote yupo shule alikuwa akipendelea kupeleka mashairi kwenye magazeti na redio. Alikuwa anapeleka magezeti ya nipashe na alikuwa anafanîkiwa kupewa nyota kwenye mashairi yake.

Wakati huo ukipeleka shairi kwenye magezeti ili upate ela lazima uwe na nyota kwenye shairi lako.na tukipewe 4000 kwa shairi.


Hakika kwa muda huo,ilikuwa ngumu kupata nyota kulinga na wimbi la watunzi wa mashairi wenye uwezo walikuwa lukuki. Mbali na kupeleka tungo zake magazetini,pia alikuwa anapeleka redio Tumaini kwenye kipindi cha 'Chimbua chimbua' ingawa huku mashairi yake mengi nayo yalipata kusomwa.


Baada ya watu kuzitambua kazi zake kwa undani,ndipo mwaka 2000,marehemu Omari Omari akakutana nae kwenye mchakato wa kutunga nyimbo za kuhamasisha timu ya taifa. Alitumia fursa hiyo kwa kumtungia nyimbo ya kuhamasisha timu yetu ya taifa.

Akiwa na Omari Omari alimtungia nyimbo nyingi sana ila kwa nyimbo ambazo zilishika soko la mashabiki ni 'Baada ya kisa mkasa','kifo cha Tx Moshi' pia kamalizi mashairi kwenye wimbo wa 'kupata majaliwa' baada Omari Omari kulianzi kutunga.

Aliingiza mijadara kwa waimbaji mnanda,kila mmoja alimuhitaji kufanya nae kazi,ndipo nae marehemu Juma Mpogo 'Lupozi' kumuhitaji afanye nae kazi. Ila sasa kwa Lupozi pale alikuwa anapiga ngoma na visoda,kisha akamtungia nyimbo ya 'mabomu mbagala' na ile ya 'mabomu gongo la mboto'.


Kwa katika kitongoji cha Temeke alikubalika na utungaji wake mzuri wa mashairi,pia anawatungia nyimbo kundi la 'Kombola' lilopo chini ya Hassani Chuna na Masiwa. Kombola nao aliwatungia nyimbo kama 'subira yavuta kheri' na kisa cha mapenzi.

Anasema kwa kipindi chote alichokuwa chini ya menejimenti ya marehemu Omari Omari na Juma Mpogo mziki wa mnanda ulikuwa ni wakipato cha chini hadi kupelekea wakienda kwenye mashoo huambulia vifedha vya maji ya kunywa na nauli ya kurudi nyumbani.

Hakika gobole amepata pigo baada ya kufa kwa marafiki wake wapendwa Omari Omari na Juma Mpogo 'Lupozi' na hivi sasa wamempoteza dira kwenye sanaa.

 Anasema kama marehemu Lupozi walipiga mkakati wa kubadiri muelekeo wa kuimba mnanda,ili waimbe taarabu kutokana na yeye gobole anaweza kutunga taarabu.

Anahisi vifo hivi vimemrudisha nyuma kutoka hivi sasa anatunga nyimbo na hamna mtu wa wakuimba.


Anaamini wangekuwepo hai marafiki zake hao,ungekuwa muda mwafaka wa wao kujipatia kipato kutokana na kipindi kile wao wanaimba mziki huu haukuwa na ela,ila kwa muda huu baada ya nyimbo zao kuchezwa kwenye kituo cha E.Fm imekuwa sapoti kubwa ya kujitangaza na kuongeza kipato ukilinganisha na zamani.

No comments:

Post a Comment