EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, January 21, 2014

Mwanza wamtaka waziri Tibaijuka kuingilia kati uhamisho wa kigogo


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini, Profesa Anna Tibaijuka
 
Wananchi wilayani Mwanza, wamemuomba Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini, Profesa Anna Tibaijuka, kuingilia kati mazingira ya uhamisho wa Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba wilayani humu, Crispin Hatson.
Kadhalika, wameomba Mwenyekiti aliyehamishwa arejeshwe ili atolee uamuzi wa mashauri yaliyokuwa katika hatua za mwisho kutokana na mrundikano wa mashauri hayo kwa sasa.

Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao, baadhi ya wananchi hao wamedai kuwa uhamisho huo umetokana na shinikizo la chuki binafsi kutoka kwa baadhi ya viongozi wake wakishirikiana na baadhi ya watu wenye uwezo wa kiuchumi kutokana na msimamo wake katika utoaji haki.

Wakizungumza nje ya jengo la Baraza hilo mwishoni mwa wiki, wananchi hao walidai kuwa baada ya uhamisho wake, baadhi ya wenye uwezo kiuchumi na vigogo wamekuwa wakitamba kwamba wamefanikisha kumng'oa.

Kwa msingi huo, wananchi hao wameiomba Wizara kumrejesha Mwenyekiti huyo hata kwa muda mfupi ili ayatolee uamuzi mashauri yao yaliyokuwa katika hatua za mwisho. 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment