EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, January 21, 2014

BARAZA LA MADIWANI MTWARA VIJIJINI LAIBUA MAKUBWA RUSHWA YAONEKANA WAZIWAZI KATIKA ELIMU



Kikao Cha Baraza La Madiwani Mkoani Mtwara Katika Halmashauri Ya Mtwara Vijijini Kilichofanyika Jana Tarehe 21-01-2014 Katika Ukumbi Wa Mikutano Wa Chuo Kikuu Cha Saint Augustini Mtwara Kimebaini Kuwepo Kwa Mkaanganyiko Mkubwa Na Hali Ya Sintofaham Katika Suala Zima La Uhamishaji Wa Walimu Kati Ya Ofisi Ya Za Kata,Halmashauru Na Ofisi Ya Katibu Tawala Wa Mkoa . Hayo Yalibainika Wakati Moja Kati Ya Watendaji Ambaye Ni Mtendaji Wa Kata Ya Kitaya Alipokuwa Akiwasilisha Taarifa Yake Ya Maendeleo Ya Kata Yake  Kwa Robo Mwaka Ya Mwisho Mwa 2013 Ambayo Imeoandaliwa Na Diwani Wa Kata Hiyo Na Katika Taarifa Hiyo Kulikuwa Na Ambatanisho La Malalamiko Ya Wakazi Wa Kata Hiyo Kuhusu Walimu Watano Kuhamishwa Kwa Awamu Tofautitofauti Na Kusiwe Na Replacement Yaani Ujazwaji Wa Nafasi Zinazoachwa Na Walimu Hao Hali Inayotishia Kushuka Kwa Kiwango Cha Ubora Wa Elimu Katika Kata Hiyo, Mara Baada Ya Kuwasirisha Taarifa Hiyo Mkurugenzi Mtendaji Wa Almashauri Ya Mtwara Vijijini MH: Iddi Mushihiri  Alisimama Na Kuomba Ruhusa Ya Mwenyekiti Kukanusha Taarifa Hiyo Kwa Maana Hajaielewa Kwa Namna Gani Waalimu Hao Wamehamishwa Na Ndipo Aliposimamishwa Afisa Elimu Wa Halmashauri Kujibia Hoja Hiyo Lakini Mara Baada Ya Afisa Elimu Huyo Kutoa Ufafanuzi Hali Haikuwa Ya Kueleweka Kutokana Na Kupishana Kwa Taarifa Zake Na Za Mtendaji Wa Kata Ya Kitaya Pia Kulionyesha Yeye Kuwa Na Taarifa Ya Mwalimu Ambaye Amehamishiwa Nanguruwe Kutokana Na Sababu Za Kiafya Hali Hii Iliibua Wasiwasi Katika Kikao Hicho Na Ndipo Mwenyekiti Wa Baraza Aliamuru Zoezi La Uwasirishaji Kusimama Kwa Muda Ili Kupisha Mazungumzo Kidogo Juu Ya Hili Na Mpaka Baada Ya Dakika Kadhaa Bado Kulionekana Kuwepo Kwa Mkanganyiko Wa Taarifa Hali Ambayo Ilionekana Kuwepo Kwa Ubabaishaji Katika Sekta Za Juu Kunako Ngazi Ya Mkoa Na Kuahidi Kulimaliza Tatizo Hilo Kwani Limekuwa Kero Inafikia Wakati Walimu Wengine Hufojiwa Nyaraka Ili Waweze Kuhama Pasipo Utaratibu.
Lakini Katika Kikao Hicho Pia Mambo Mengine Yaliyozungumzwa Ni Hali Ya Kiutendaji Kwa Madiwani Katika Shughuli Za Kimaendeleo Ambapo Imeonekana Kuwa Nziuri Nay A Kuridhisha Kwani Mambo Mengi Mazuri Yamefanywa Na Maendeleo Yamepatikana Huku Mkurugenzi Akitolea Ufafanuzi Swala La Ujenzi Wa Mfumo Wa Maji Wa Mbuo Kwamba Haujakwama Na Vifaa (Mabomba) Vimeshafika Hivyo Mkandarasi Yuko Site Kwa Ujenzi Mara Baada Ya Kurejea Toka Mapumzikoni Tofauti Na Ilivyoeleza Taarifa Ya Mtendaji Wa Kata Hiyo Kuwa Mkandarasi Wa Mradi Huo Wa Maji Amekimbia Au Kutoweka Katika Mradi Huo Pasipo Mradi Kukamilika.

No comments:

Post a Comment