EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, October 22, 2013

WANAFUNZI ELIMU YA JUU KUPATA MIKOPO YA BILLIONI 3.2



Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi na bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu hapa nchini, zitawapa mikopo inayofikia kiasi cha sh. Bilioni 3.1 wanafunzi 1,107 kutoka katika bajeti zao, baada ya wanafunzi hao kulalamika kukosa mikopo.
Naibu waziri wa elimu Tanzania Philipo Mulugo
 Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi, philipo mulugo, ambaye amesema kuwa baada ya kutafakari suala hilo, uamuzi umefikiwa kuwa wanafunzi hao waitwe kujaza tena fomu za kuomba mikopo.

 Takriban wiki mbili zilizopita, zaidi ya wanafunzi 100 waliochaguliwa kujiunga katika vyuo vikuu mbalimbali nchini kwa mwaka huu, waliandamana kwenda wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi, kwa lengo la kukutana na waziri mwenye dhamana na wizara hiyo, dk.shukuru kawambwa, baada ya kukosa mikopo.Wanafunzi hao walisema wamenyimwa mikopo bila kupewa maelezo ya msingi licha ya kuilalamikia bodi ya mikopo.Uamuzi huo wa jana, umekuja baada ya kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za jamii, kuzibana wizara na bodi, ikitaka kujua kilichosababisha wanafunzi hao kukosa mikopo. Naibu waziri huyo amesema kuwa bodi itatakiwa kutafuta fedha hizo kutoka kwenye matumizi mengine, na kutumia fedha za marejesho ya mikopo kugharimia wanafunzi hao. Wanafunzi watakaofaidika ni wale wanaochukua masomo ya ualimu wa hisabati (20), ualimu sayansi (164), udaktari tiba (111) na uhandisi umwagiliaji (7), wengine ni ualimu (617), sayansi kilimo (20), uhandisi (70) na sayansi ya jamii (98).

No comments:

Post a Comment