EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Monday, January 20, 2014

KASHESHE YAZUKA BAADA YA WANANCHI KUGUNDUA UBADHILIFU MKUBWA WA FEDHA ZA MAPATO YA MWAKA 2013 KIJIJI CHA NALIENDELE MKOANI MTWARA

WANANCHI WA NALIENDELE MTWARA
NA: MUBA.S MUBA
mkutano wa kijiji naliendele mkoani mtwara ulikuwa ufanyike mwezi oktober mwaka jana na hatimaye kupangwa kufanyika siku ya tarehe 16 january mwaka huu lakini haukukamilika mara baada ya wajumbe kutokamilika katika awamu hiyo ya mkutano huku wajumbe 92 ndio waliokuwa wamewasiri katika eneo la kikao kati ya wajumbe wote ambao ni 7275 wakazi wa kijiji hicho. serikali ya kijiji ililazimika kupanga tarehe nyingine ya mkutano huo ambayo ilikuwa ni tar 18-january 2014 jumamosi na hatimaye mkutano huo kufanyika kama ilivyopangwa baada ya wajumbe 252 kati ya wajumbe 7275 waliotakiwa kuwepo hivyo serikali ya kijiji kujiridhisha na idadi hiyo ya wajumbe na kuamuru mkutano kuendelea,kikao hicho kilichokuwa na ajenda 7 ambapo ya kwanza ni kufungua mkutano,
ya pili ni kusoma taarifa iliyopita,yatokanayo,taarifa za miradi mapato na matumizi,mengineyo na ajenda ya mwisho ni kufunga mkutano huku ajenda kubwa katika mkutano huo ikiwa ni ajenda ya mapato na matumizi ambayo ilitiliwa shaka na wananchi kabla ya kikao na hii ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya wananchi kususia mkutano wa wali kwa madai kuwa serikali yao ya kijiji inajaribu kuwaficha ukweli kuhusu mapato na matumizi ya mwaka 2013 huku hoja zikiibuka mara baada ya wadau muhimu katika kijiji hicho kushindwa kuonekana katika mkutano huo muhimu kwa maendeleo yao. wadau hao ni kama vile kaimu mwl mkuu wa shule ya msingi ,mwl mkuu wa sekondari pamoja na mtendaji wa kata wakiwamo wafanyakazi wa chuo cha kilimo cha naliendele, lakini mara baada ya kusomwa kwa ajenda ya mapato na matumizi wananchi wote walikataa kupokea taarifa hiyo baada ya kugundua kuwa ilikuwa na mapungufu makubwa hivyo mara baada ya wananchi kukataa kupokea taarifa za mapato na mtumizi kikao hicho kilighairishwa na kimepangwa kufanyika tarehe 30 january mwaka huu huku wananchi wakiwataka viongozi kuwa siku hiyo watoe taarifa sahihi na kama wakishindwa basi wawajibike.mkutano wa mwisho kufanyika na kuzungumzia mapato na matumizi ya kijiji hicho ulikuwa i tarehe 17-04-2013 hivyo toka mwezi huo mpaka siku ya jumamosi january 17 -2014 serikali ya kijiji imekusanya fedha mill 3 laki 6 arobain na nne elfu 892 na sent 70 na matumizi ni mill 3na 75 na fedha liliyobaki ni laki sita 79 elfu na 70 na ndipo mzozo ulipoanza kijiji hicho kwa sasa kimekuwa na mizozo isiyomalizika kwani bado kuna kesi inayoendelea mahakamani ikimtuhumu ndg chihipo kuvunja choo kilichojengwa na kijiji kwa maana eti kimejengwa chini ya kiwango.

No comments:

Post a Comment