EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, January 7, 2014

CAF YAMPA LESENI YA HADHI YA JUU KOCHA JULIO



                                  ALIYEKUWA kocha Msaidizi wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Jamhuri Mussa Kihwelo ‘Julio’ ametunukiwa leseni ya daraja B ya ufundishaji kandanda na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), baada ya kuhitimu vizuri mafunzo yaliyofanyika mwaka jana visiwani Zanzibar.
KIHWELU 
Julio aliyekuwa Msaidizi wa mchezaji mwenzake wa zamani wa Simba SC, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’  walifukuzwa baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu msimu na nafasi zao kuchukuliwa na Mcroatia Zdravko Logarusic na mzalendo Suleiman Matola ‘Veron
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine leo amemkabidhi Julio leseni yake pamoja na za makocha wote wengine walioshiriki kozi iliyofanyika mjini Zanzibar mwaka jana ambao hawakuwepo.
Makocha wengine waliofuzu kozi hiyo iliyoendeshwa na mkufunzi Bhekisisa Boy Mkhonta kutoka Swaziland ni Abdulghan Msoma, Hafidh Badru, Nasra Juma Mohamed, Gulam Abdallah Rashid, Mohamed Ayoub Suleiman, Shaaban Ramadhan, John Simkoko na Hemed Suleiman Ali. Hivi sasa Tanzania ina makocha 40 wenye leseni B za CAF baada ya wengine 31 kufuzu katika mafunzo yaliyofanyika mapema mwaka juzi jijini Dar es Salaam chini ya mkufunzi Honor Janza kutoka Zambia.

No comments:

Post a Comment