EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, December 25, 2013

Kocha wa makipa wa club ya Simba “James Kisaka” afariki dunia.

KIPA wa zamani wa klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam, James Kisaka amefariki dunia asubuhi ya leo katika hospitali ya Burhan, Dar es Salaam.
FFFFF
MAREHEMU KISAKA JAMES
Habari ya kuhuzunisha kwenda wapenzi wa soka hasa wa club ya Simba ni kuhusu msiba wa James Kisaka.
Kisaka amefariki dunia leo asubuhi kwenye hospitali ya Burhan.
James Kisaka alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya macho,kichwa na miguu kwa muda mrefu.




James Kisaka alizaliwa mwaka 1955 mjini Dar es Salaam na alipata elimu yake ya Msingi katika shule ya Oysterbay na baadaye sekondari za Mzizima na Tambaza, Dar es Salaam pia.
Alianza kupata umaarufu wa soka tangu anasoma na haikushangaza aliposajiliwa na Sigara akiwa kijana mdogo chini ya umri wa miaka 20.
Baadaye alichezea Nyota Nyekundu, Simba SC, Small Simba ya Zanzibar, Volcano ya Kenya alipokwenda na Zamoyoni Mogella na LiIa Shomari (pia marehemu) na Ndovu ya Arusha.
Alikuwemo kwenye kikosi cha Simba kilichokwenda ziara ya mafunzo nchini Brazil mwaka 1981.
Kisaka atakumbukwa kwa upole wake na ufanyaji kazi kwa bidii enzi za uhai wake. Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Ami


379712_654492864594135_585974560_n

No comments:

Post a Comment