EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Sunday, November 3, 2013

VILLA SQUAD YATOKA 11 NA JUHUDI FC

TIMU ya soka Villa Squad ya Magomeni, juzi ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Juhudi Fc ya Mabibo katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa shule ya msingi Makurumla Mwembechai.
Juhudi ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 10 kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo huo kupitia mshambuliaji wake Salgado Kipara na kuzifanya timu hizo kwenda mapumziko Juhudi wakiwa mbele kwa bao hilo.
Kipindi cha pili timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu kila moja ikikosa nafasi za wazi kutokana na washambuliaji wa pande zote kukosa umakini wa umaliziaji.
Dakika ya 79 Omari Mohamed alifanikiwa kuisawazishia timu yake ya Villa Squad bao baada ya kuwatoka mabeki wa timu pinzani na kuachia shuti kali lililojaa wavuni moja kwa moja.
Baada ya mchezo huo kumalizika kocha mkuu wa Juhudi FC,Kaduguda Reuben alisema kuwa timu yake ilicheza vizuri ila hawakuwa na bahati ya kuibuka na ushindi.
“Wachezaji wangu walijitahidi kucheza vizuri kwa dakika zote 90 ila bahati haikuwa upande wetu,mwamuzi alichezesha vizuri sana ndio mana hapakuwa na malalamiko kutoka kwa pande zote,” alisema.

No comments:

Post a Comment