EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Sunday, November 3, 2013

VYAMA VYA SOKA MIKOANI KUANZISHA LIGI YA WANAWAKE

NA MSHAM, NGOJWIKE
UONGOZI wa vyama vya Soka mikoani umeshauriwa kuanzisha Ligi ya wanawake kwa ajili ya kuendeleza na kukuza mchezo huo ambao uneonekana kuwa ni wa wanaume pekee.
Ombi hilo limetolewa na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya wasichana chini ya miaka 17 ‘Tanzanite’ ambayo inashiriki kwenye michuano ya kusaka tiketi ya mucheza fainali za kombe la Dunia zitakazochezwa mwakani nchini Canada.
Akizungumza na BINGWA juzi kocha huyo alisema kuwa ni muhimu kuhamasisha soka la wanawake hasa kwa kuanzia mikoani kwa kuanzisha Ligi ndogo ndogo ambazo baadaye kupata timu zinaoeleweka na kuzisajili.
“Hatuwezi kupata jibu la kwanini soka la wanawake halipewi kipaumbele hadi pale tutakapoamua kutafuta njia za kuliinua na kuliendekeza kuanzia mikoani” alisema.
Kaijage alisema kwamba mchezo huo umeonekana kuwa kama ni wa wanaume pekee ambapo inawafanya hadi na wasichana wenyewe wanaoshiriki mchezo huyo kutaka kujifananisha na wanaume.
Tanzanite kwa sasa inaendelea kujiandaa na mechi yao ya marudiana dhidi ya timu ya Taifa ya Msumbiji itakayochezwa hivi karibuni nchini humo, baada ya kushinda katika mechi yao ya kwanza iliyochezwa Oktoba 26 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment