EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Sunday, November 3, 2013

MLALO STARS YADHAMIRIA KUTETEA UBINGWA WAO

NA MSHAM NGOJWIKE
TIMU ya soka ya shule ya Sekondari Mlalo Day (Mlalo Stars), ya Wilayani Lushoto imedhamiria kutetea ubingwa wao wa michuano ya Shambalai Cup inayoendelea katika jimbo hilo la Mlalo.
Akizungumza na SWACO jana kutoka Lushoto,mwalimu wa michezo wa shule hiyo,Fineas Mashombela alisema kwamba ameiandaa timu yake kikamilifi kuhakikisha ubingwa unatua mikononi mwao tena.
“Ligi imeshaanza lakini sisi bado hatujaanza kucheza kwani ndio mabingwa watetezi tunasubiri mpaka raundi ya pili,kwa ujumla nimekiandaa kikosi changu kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu,” alisema.
Alisema moja ya mambo anayoyafanyia kazi ni safu yake ya ushambuliaji ili kufunga mabao mengi zaidi kuliko msimu uliomalizika na pia safu yake ya ulinzi isiruhusu mabao ya kizembe.
“Kwa sasa kitu ambacho ninakifanya ni kuisuka safu yangu ya ushambuliaji ili kupata mabao mengi zaidi na pia safu ya ulinzi isije ikaruhusu mabao ya kizembe,kwa ujumla naamini hakuna kitakachoharibika,” alisema.
 

No comments:

Post a Comment