EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Sunday, November 3, 2013

MBEYA CITY YATOA TAMKO JUU YA KASI YAO

NA ,MSHAM NGIJWIKE
MSHAMBULIAJI wa Mbeya City,Paul Nonga amesema kuwa wale wanaodhani kasi ya timu yao ni nguvu ya soda watafunga midomo yao ligi itakapomalizika.
Mbeya City ambayo imepanda daraja msimu huu imekuwa mwiba mchungu kwa timu zinazoshiriki ligi kuu ambapo mpaka sasa wanashika nafasi ya pili wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja.
Akizungumza na BINGWA jana kutoka jijini Mbeya,Nonga alisema kuwa baadhi ya watu wanafikiri timu yao itapunguza kasi mbele ya safari kwani ndio kwanza wamepanda daraja lakini akasisitiza kwamba lengo lao ni kuchukua ubingwa.
“Watu wengi wanadhani kwamba kasi tuliyonayo itakuja kupungua mbele ya safari lakini mimi nawaambia tumedhamiria kuchukua ubingwa msimu huu licha ya kwamba ndio kwanza tumepanda daraja,” alisema. 
Nonga ambaye alisajiliwa na timu hiyo akitokea kwa JKT Oljoro ndiye anayeongoza katika timu hiyo kwa kufunga mabao ambapo ameshafunga mabao manne mpaka sasa.
Mbali na kudai timu yake itaibuka bingwa msimu huu,pia Nonga amesema kwamba dhamira yake ni kuibuka mfungaji bora na kuwafunika Amis Tambwe wa Simba anayeongoza pamoja na Hamis Kiiza wa Yanga.
 

No comments:

Post a Comment