EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Sunday, November 3, 2013

AABA YAANDAA MASHINDANO YA UHURU MKOANI ARUSHA

NA EZEKIEL TENDWA
CHAMA cha ngumi Mkoani Arusha (AABA) kimeandaa mashindano yajulikanayo kama Uhuru Cup yatakayoshirikisha timu za ukanda wa Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika Desemba 9 hadi 12 jijini Arusha.
Akizungumza na BINGWA jana kutoka jijini Arusha,Katibu mkuu wa AABA,Mohamed Abubakar alisema kuwa maandalizi yanakwenda vizuri huku wakipata sapoti kubwa kutoka kwa wadau mbalimbali.
“Tutakuwa na mashindano ambayo tumeyapachika jina la Uhuru Cup yanayotarajiwa kufanyika tarehe 9 hadi 12 mwaka huu hapa Arusha na jambo la kushukuru tunapata sapoti kubwa kutoka kwa wadau mbalimbali,” alisema. 
Alisema baadhi ya timu ambazo zinatarajiwa kushiriki mashindano hayo ni timu kutoka Kampala nchini Uganda,Nairobi pamoja na Mombasa kutoka nchini Kenya,Mwanza,Dar es Salaam pamoja na wenyeji Arusha. 
Katika hatua nyingine alisema kwamba wanatarajia mabondia wao wataonyesha mchezo mzuri kama walivyofanya katika mashindano ya majiji yaliyofanyika Nairobi Kenya mwanzoni mwa mwezi uliopita.
“Mwanzoni mwa mwezi uliopita katika michuano ya majiji yaliyofanyika Nairobi nchini Kenya tulifanikiwa kuibuka na medali tatu sasa kipindi hiki tupo nyumbani tutafanya vizuri zaidi,” alisema.

No comments:

Post a Comment