NA MSHAMU NGOJWIKE
TIMU 56 za Ligi Daraja la
Tatu na Nne za Wilaya ya Temeke Zimethibisha kuchukua fomu huku ikiwa na
upungufu wa timu shiriki liogi daraja la tatu.
Ligi daraja la tatu na nne ngazi ya wilaya ya
temeke linarajiwa kuanza novemba 2 amabalo litachezwa kwenye viwanja sita ndani
ya wilaya hiyo.
Akizungumza na BINGWA Katibu
wa Chama cha mpira wilaya ya Temeke(TEFA)Khassim Mustapha Alisema Timu 40 ligi
daraja la nne zimechukua fomu hizo, huku timu 16 pekee za ligi daraja la tatu
zilizochukua fomu hizo na wakiwa na upungufu wa timu nne kama kanuni inavyotaka ya kuwa na timu
zisizo pungua 18 na zisizo zidi 20.
"hadi sasa na timu za
ligi la daraja la nne maana tuna timu 40 na zinatosha kwa ligi yetu, lakini kwa
ligi daraja la tatu tuna timu chache hadi
leo timu ambazo zimechukua fomu za ushiriki ni 16 tu" alisema.
Alisema viwanja ambavyo
vitatumika kwenye ligi hiyo pamoja na Mzinga jeshini kigamboni,Makangarawe
uliopo Yombo,Twalpo Jkt,Mivinjeni wa Shule ya Sekondari Kurasini,Gonga Kongowe
na Chamanzi Uliopo Shule ya Msingi Chamanzi.
No comments:
Post a Comment