EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, October 28, 2016

KAULI YA FERGUSON JUU YA UBINGWA EPL 2016/2017 YAWATIA WAZIMU PEP, NA MOURINHO

MENEJA LEKENDARI Sir Alex Ferguson anadhani Manchester City ndio wenye nafasi kubwa kutwaa Ubingwa wa England Msimu huu huku akiwa kimya kuhusu nafasi ya Kikosi cha Chelsea chini ya Meneja wao Antonio Conte.
Sir Alex Ferguson, mwenye Miaka 74, aliongea hayo akiwa huko Nurenberg, Germany alikokwenda kupokea Tuzo ya Walther Bensemann ambayo hutunukiwa Watu waliotoa Utumisha Uliotukuka kwenye Soka.
Tuzo hiyo hutolewa kwa ajili ya Kumbukumbu ya Bensemann ambae ndie anasemekana ni Muasisi wa Soka la Germany ambae alianzisha Jarida la Michezo, Kicker, Mwaka 1920.

Baadhi ya Washindi waliopita waliowahi kutwaa Tuzo hii ni pamoja na Franz Beckenbauer, Alfredo di Stefano and Sir Bobby Charlton.
Akiongea na Jarida la Kicker, Sir Alex Ferguson, ambae alistaafu Umeneja Man United Mwaka 2013 baada ya kuiongoza kwa mafanikio makubwa kwa Miaka 26 akitwaa Makombe 38, amezitaja Timu 5 zenye nafasi nzuri za kuwa Mabingwa wa EPL, Ligi Kuu England.

Ferguson alisema: “Nadhani wapo Wagombea Watano. Man City wao ndio wana nafasi kubwa, Tottenham na Liverpool pia, lakini Man United pia wamo ikiwa tutapata mtiririko mzuri hivi karibuni.”
Aliongeza: “Hata kama unalegalega nyuma kwa Pointi 6 au 8 bado inawezekana kuzikamata Timu 2 au 3!”
“Ushindani na uzoefu kati ya Guardiola na Mourinho utaleta upinzani mzuri wa kuvutia. Msiisahau Arsenal. Timu imeimarika sasa. Wamekuwa bora na wakali. Nimefurahishwa sana na Chipukizi wao Alex Iwobi!”
Pia Ferguson anaamini ufundi wa Bosi wa Manchester City Pep Guardiola hauwezi kujadiliwa licha ya sasa kwenda Mechi 6 bila ushindi.
Vilevile, Ferguson alimsifia Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino, na kumsema ana uwezo mkubwa.
Alisema: “Mauricio Pochettino anao uwezo na Spurs ina mchanganyiko mzuri wa Vijana na wale Wazoefu. Wachezaji wao wakubwa, Harry Kane na Eric Dier, ni majeruhi lakini bado wapo nafasi nzuri!”
Mbali ya kudai kuwa Meneja wa Chelsea Antonio Conte ameirejesha Chelsea juu wanapostahili, Ferguson hakueleza lolote kuhusu nafasi ya Chelsea Msimu huu.
EPL - LIGI KUU ENGLAND
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 29
1430 Sunderland v Arsenal         
1700 Man United v Burnley
1700 Middlesbrough v Bournemouth                
1700 Tottenham v Leicester        
1700 Watford v Hull
1700 West Brom v Man City       
1930 Crystal Palace v Liverpool             
Jumapili Oktoba 30
1630 Everton v West Ham 
1900 Southampton v Chelsea                
Jumatatu Oktoba 31
2300 Stoke v Swansea               

No comments:

Post a Comment