EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, October 15, 2013

KENYA YAJIPANGA KIJESHI



Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema serikali yake italifanya jeshi la Kenya na zana zinazotumiwa na jeshi ziwe za kisasa, ili kukabiliana na mashambulizi yanayoweza kutokea.\
Raisi wa kenya uhuru kenyata

Rais Kenyatta amesema hayo wakati Kenya ikiendelea kutafakari ni kwanini idara za usalama, zilichukua muda wa siku nne kushughulikia tukio la kigaidi la Westgate lililotokea Septemba 21 mjini Nairobi.
Kwa sasa Kenya inaendelea kukabiliana na tishio la usalama kutoka kwa kundi la Al Shabaab.Hapo Jana Polisi wa Kenya walisema wamewakamata watu wawili wanaohusika kulisaidia kundi la Al Shabaab.
Mmoja ni Juma Kisatu anayetuhumiwa kuwashawishi vijana kujiunga na kundi la Al Shabaab, na mwingine ni Osman anayetuhumiwa kutoa fedha kwa kundi hilo.

No comments:

Post a Comment