EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, October 16, 2013

JACKOB ZUMA ASHAURI MACHAFUKO AFRIKA YA KATI KUCHUKULIWA HATUA

Jackob Zuma Rais wa afrika kusini
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za kivitendo kwa shabaha ya kuhitimisha machafuko katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Rais Zuma ametangaza kuwa, Afrika Kusini na Ufaransa ziko tayari kushirikiana na Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa minajili ya kuhitimisha machafuko na ukosefu wa usalama katika nchi hiyo.
Rais wa Afrika Kusini amesisitiza kwamba, serikali ya Bangui inapaswa kutoa ushirikiano wa lazima ili kuhakikisha kwamba, amani na usalama vinarejea tena katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Rais Zuma amesema hayo katika mazungumzo yake ya Rais Francois Hollande wa Ufaransa aliyeitembea Afrika Kusini. Hollande amesema katika mazungumzo hayo kwamba, Paris ina wasi wasi wa hali hiyo ya ukosefu wa amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kuenea pia katika nchi jirani na nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment