EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, October 15, 2013

MAKTABA YA MKOA WA MTWARA HAITUMIWI NA WALENGWA



WANAFUNZI wa Manispaa ya Mtwara Mikindani wametoa maoni yao, juu ya matumizi ya maktaba ya mkoa, iliyopo maeneo ya maduka makubwa mjini Mtwara, na kuomba utaratibu wa kuingia na kutoka katika maktaba hiyo uwekwe bayana.
Wakizungumza na mwandishi wa Pride Fm Redio katika eneo la maktaba
hiyo, mmoja wa wanafunzi hao kutoka shule ya sekondari ya Chuno Mohamed Mussa amesema kuwa, ni vyema maktaba ikatoa utaratibu wa wananfunzi wa kuingia katika maktaba hiyo, kutokana na maktaba ya shule yao kutokidhi mahitaji ya wanafunzi hao.
Aidha Mohamedi ameongeza kuwa na ni vyema kwa uongozi wa shule ya Sekondari ya Chuno ukafutilia utaratibu wa maktaba hiyo ya Mkoa, ili kuwapa wanafunzi utaratibu utakaokuwa pale na hiyo itawapatia nafasi za kujifunza zaidi.

Mwanafuzi mwingine kutoka shule ya sekondari Shangani Walivyo Fadhil, amesema kuwa ni vyema kwa maktaba ya Mkoa ikatoa fursa za eneo hilo la utaratibu, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kutanua wigo wa wanafunzi wa shule zote zilizopo katika mkoa wa Mtwara kujisomea.
ENDELEA ZAIDI

No comments:

Post a Comment