EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, October 12, 2013

AFRIKA WAIKAZIA ICC



Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya makosa ya jinai ICC Fatou Bensuda

Viongozi wa Afrika wameikosoa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu - ICC kwa kulilenga bara la Afrika katika kesi zake.
Viongozi hao pia wameitaka mahakama ya ICC izifute kesi dhidi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.
Kenyatta na Ruto wanakabiliwa na mashitaka ya uhalifu wa kivita kuhusiana na machafuko yaliyozuka baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007, uliofuatiwa  na   ghasia zilizosababisha vifo vya  watu zaidi ya 1,000.Matamshi hayo yametolewa katika siku ya kwanza ya Kikao maalum cha siku mbili cha Umoja wa Afrika,  katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa.Umoja wa Afrika wenye nchi  wanachama 54, uliitisha kikao hicho maalum ili kujadili mahusiano yao na Mahakama ya ICC, na pia kumchagua Kamishina mpya wa amani na usalama wa umoja huo.

No comments:

Post a Comment