EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, October 12, 2013

ITALIA YAENDELEA NA KILIO CHA WAHAMIAJI



Wakimbizi kadhaa wanahofiwa kuwa wamekufa baada ya  mashua yao kuzama karibu na kisiwa cha Sicily, katika bahari ya Mediterenia nchini Italia.
papa fransisco

Watu 250 wanasemekana kuwa walikuwamo katika mashua  hiyo iliyozama umbali wa maili 70, kutoka pwani ya kisiwa cha Italia cha Lampedusa. Shirika la Habari nchini Italia Ansa, limesema takribani miili 50 ikiwa ni pamoja na wanawake na karibu watoto 10, imeondolewa baharini.
Waziri Mkuu wa Italia Enrico Letta, amesema kiasi ya manusura 150 wameokolewa na meli nyingine ya Malta.
Wiki iliyopita wakimbizi zaidi ya mia  tatu  walikufa maji karibu na  kisiwa hicho cha Lampedusa.Mashua  hiyo  iliyokuwa inawasafirisha wakimbizi mita tano ambao wengi wao ni kutoka Eritrea na  Somalia ilizama baada ya kuwaka  moto.

No comments:

Post a Comment