EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, October 12, 2013

WAISLAM MAKKA WAENDELEA NA HIJJA


waumini wa kiislam wakiwa katika ibada Makka

Maelfu ya mahujaji wa kiislamu wamekusanyika katika mji mtukufu wa Makka nchini Saudi Arabia katika ibada ya kila mwaka ya Hajj, huku maafisa wa nchi hiyo wakionya dhidi ya kuingizwa siasa ndani ya mkusanyiko huo mkubwa duniani.
Imam wa msikiti mkuu wa Makka Sheikh Saleh bin Mohammed al-Taleb, amewataka waislamu duniani kote kuungana pamoja na kumaliza mizozo.
Hijja ni nguzo ya  mwisho katika nguzo tano za Uislamu inayomhimiza kila mwenye uwezo kufanya Hijja,
 
Msikiti mtukufu wa Mkka
kufanya hivyo angalau mara moja maishani mwake.Maafisa nchini humo wanasema tayari mahujaji takriban milioni 1.4 wameshawasili kwa ibada hiyo, ingawa idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na mwaka uliopita ambapo takriban mahujaji milioni 3.2 walihudhuria.
Inasemekana Matatizo ya kupumua kutokana hali mbaya ya joto ni moja wapo ya  sababu za  kupungua kwa idadi ya mahujaji mwaka huu.

No comments:

Post a Comment