EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Monday, August 5, 2013

MKE WA MTU ANUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUNASWA AKIIBA NGUO KARIAKOO


Jimama mwenye hadhi yake ambaye ni mke wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Mary au Mama Gilo, mkazi wa Sinza jijini Dar amekula kichapo cha kutisha almanusra apoteze uhai baada ya kunaswa akiiba nguo kwa ajili ya Sikukuu ya Eid El Fitr. Tukio hilo la aibu lililoshuhudiwa na  mwandishi wetu lilijiri katika moja ya maduka makubwa ya nguo Kariakoo, Dar mwishoni mwa wiki iliyopita. Mama Gilo ambaye anafahamika Kariakoo na Sinza, alinaswa akiiba nguo za sikukuu ikiwa ni pamoja na ‘madira’ ya kumalizia mfungo. Katika tukio hilo lililokusanya kadamnasi, mwanamke huyo alipigwa chabo kwenye duka la mfanyabiashara Rehema Kessy...

MUME AUWAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI BAADA YA KUMNYONGA MKEWE

MWANAMUME mmoja amemnyonga hadi kufa mke wake na yeye akauawa na wananchi wenye hasira, katika Wilaya ya Bunda mkoani Mara. Tukio hilo lililothibitishwa na polisi wilayani hapa, lilitokea usiku wa kuamkia juzi katika Kijiji cha Kisangwa Kata ya Mcharo, kwenye sherehe ya ufunguzi wa nyumba ya ndugu yao.Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mcharo, Waziri Kingi, alimtaja mwanamke aliyeuawa kwa kunyongwa na mume wake kuwa ni Paulina Samson Misinzo. Kingi alimtaja mwanamume huyo ambaye pia aliuawa na wananchi wenye hasira, baada ya kukimbilia mlimani kuwa ni Batule Masanja, mkazi wa kijiji hicho.Imeelezwa kuwa siku ya tukio mwanamume huyo aliyekuwa...

No comments:

Post a Comment