kibaka aliyekamatwa akiwa na baadhi ya raia wenye hasira wakimtoa bomani kabla ya kifo chake |
Kwa mujibu wa maelezo ya mashuhuda (kassian Mpangala) walioko
katika eneo la tukio wamesema kuwa mwizi huyo ambaye mpaka saa hizi
hajajulikana jina lake alikamatwa majira yasaa kumi na moja alfajiri mitaa ya Jeti
kwa Gude Airpot jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akijaribu kuiba Redio
ndani ya moja ya nyumba ya mkazi wa eneo hilo na muda mfupi baadae wenye nyumba
walishtuka hata kabla hajafanikiwa kutimiza tukio lake hilo na walipiga mayowe
na kujaza watu nkibao ambao walianza kumshambulia mwizi huyo kwa mawe na
magongo ingawa alifanikiwa kuwatoroka na kujificha kwenye boma ambalo
linajengwa na baadae wananchi walilizingira boma hilo na kibaka huyo kuzidiwa
nguvu,kwa tukio hilo walimtembezea kichapo kilichopelekea kifo chake Askari wa
kituo cha polisi cha kati cha Airpot walifika eneo la tukio majira ya saa moja
asubuhi na kuukuta mwili wa kibaka huyo ukiwa umetelekezwa mahali hapo huku
akiwa `tayari amefariki na hakukuwa na mtu yeyote aliyekutwa eneo la tukio.
AM NOT INVISIBLE - BOLT.
AM NOT INVISIBLE - BOLT.
GAZZA AWEKWA LUPANGO KWA ULEVI.
MSHAMBULIAJI nyota wa
zamani wa kimataifa wa Uingereza, Paul Gascoigne maarufu kama Gazza
amekamatwa baada ya kufanya fujo wakati amelewa katika kituo cha treni. Gazza
mwenye umri wa miaka 46 ambaye ametoka kupatiwa matibabu ya kunywa
pombe kupindukia nchini Marekani mapema mwaka huu alishikiliwa na polisi
baada ya kufanya tukio hilo huko Hertfordshire. Msemaji
wa Polisi wa eneo hilo alithibitisha kuwa wamemkamata nyota huyo wa
zamani baada ya kupigiwa simu na mlinzi wa eneo la kituo cha treni
kwamba anafanya fujo kutokana na kulewa pombe kupitiliza. Msemaji
huyo aliendelea kudai kuwa walimshikilia Gazza kwa saa 12 na baadae
kuwekewa dhamana na uchunguzi wa polisi unaendelea kuhusiana na tukio
hilo kabla ya kupelekwa mahakamani. Mapema
mwaka huu baadjhi ya wachezaji walijichangisha na kupata fedha ambazo
zilimsadia Gazza kumpeleka Marekani kwa ajili ya matibabu ya kuzuia
ulevi uliopindukia baada ya hali yake kuwa mbaya.
No comments:
Post a Comment