Vilio na simanzi vilitanda Jumatano iliyopita Mwananyamala
Kisiwani, jijini Dar kufuatia mtoto wa mwaka mmoja, Rahim Rajab kufariki
dunia kwa kuangukiwa na watu watatu, akiwemo baba yake mzazi, Rajab
Said..
Tukio la watu hao
kumwangukia mtoto huyo lilitokea Jumatatu iliyopita na lilisababishwa na
ugomvi mkubwa wa CD yenye nyimbo za mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond’ ulioibuka ndani ya chumba cha kulala kati ya mama wa
marehemu na mpangaji mwenzake aitwaye Aisha.
Akizungumza
kwa machungu kuelezea tukio hilo, mama mzazi wa marehemu Rahim, Habiba
Ally alikiri kuwa kisa cha kifo cha mwanaye ni...
NELSON MANDELA YUKO KATIKA HALI YA "USINGIZI WA KUDUMU"....NYARAKA ZAFICHUKA
Nelson Mandela ameendelea kuwekwa
hai kwa msaada wa mashine za kumsaidia kupumua na
'anakaribia kifo,' nyaraka za mahakama zimefichua.
Afya
ya rais huyo wa zamani ni 'yenye hatari kubwa,' kwa mujibu wa nyaraka
zilizowasilishwa mahakamani kwenye kesi ambayo imepelekea mabaki ya
miili ya watoto wake watatu kuzikwa upya Alhamisi kwenye makaburi yao ya
awali.
Nyaraka za mahakama za Juni 26 zilisema: "Matarajio hayo ya
kukaribia kifo chake yanaegemea katika uhalisia na uthabiti,' zilisema
nyaraka hizo za mahakama.
Mandela, ambaye alilazwa hospitali Juni 8,
ameendelea kuwa mahututi lakini hali inayoimarika, kwa mujibu...
LOWASSA AVIONYA VYOMBO VYA DOLA...!
WAZIRI Mkuu mstaafu, Edward Lowassa amevitaka vyombo vya dola
na wafanyabiashara wakubwa nchini, kujenga mahusiano bora kati yao na
wafanyabiashara ndogo ndogo (Machinga) ili kuondoa tabaka la matajiri na
masikini linaloweza kuathiri uchumi wa taifa.
Lowassa
aliyasema hayo jana wakati akizungumza na machinga wa eneo la Makoroboi
jijini Mwanza, ambao pamoja na mambo mengine aliwachangia sh milioni 20
kwa ajili ya kutunisha mfuko wao.
Mwanasiasa
huyo ambaye pia ni mbunge wa Monduli, aliinyoshea kidole Serikali ya
chama chake cha Mapinduzi (CCM) na kuitaka ihakikishe inatekeleza kwa
vitendo ilani yake inayosisitiza wananchi kuwezeshwa...
PICHA CHAFU ZA MISS UNIZIK ZASAMBAA MITANDAONI....
Vituko vya mapenzi ya Tz kumbe hata nchi za nje vipo..!!
Huyu ni denti wa chuo kikuu cha UNIZIK kilichoko Nigeria ambaye pia ni miss UNIZIK 2013/2014....
Mrembo huyu amekutana na balaa hili baada ya mpenzi wake kuzisambaza picha zake za utupu....
Taarifa toka chuoni hapo zinadai kuwa, wapenzi hao walizunguana siku kadhaa baada ya mrembo huyo ...
"MWANAUME ASIYE NA PESA HAPASWI KUWA NA WIVU KWA MPENZI WAKE"....JINI KABULA
MSANII wa filamu za Bongo, Miriam Jolwa ‘Kabula’ ameonesha kukerwa na
wanaume ambao hawana hela lakini wamekuwa wakijifanya
wanajua kupenda sana huku wakiwa na wivu kupitiliza.
Akiongea na mwandishi wetu , Kabula alisema anajua kupenda
ni suala la msingi lakini anawashangaa wale wanaokuwa na wivu wa
kupindukia na wakati mwingine kutoa vipigo kwa wapenzi wao wakati wao ni
wanaume wasio na kitu.
“Unajua nawashangaa sana wanaume wa aina hiyo,
wanakuwa na wivu kupitiliza lakini hawawasaidii chochote wapenzi wao kifedha
zaidi ya kuonesha wana wivu na wakipishana kidogo tu kipigo
kinatembea, mimi...
WAZIRI MAGUFULI ATAMANI KUWA RAIS WA TANZANIA......ANADAI KWAMBA YUPO TAYARI KUGOMBEA MWAKA 2015 ENDAPO ATAKIDHI MASHARTI
Katika hali inayoonyesha kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli,
anautamani urais, amesema anaweza kutangaza nia hiyo kama atakidhi
masharti yatakayowekwa kwenye Katiba mpya.
Alisema iwapo Katiba ijayo itakuja na sifa ambazo atakidhi vigezo kuna
uwezekano mkubwa wa kuwania nafasi hiyo na kwamba iwapo atapungukiwa
sifa zinazohitajika kwa mujibu wa Katiba hataingia kwenye kinyang’anyiro
hicho.
Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato alitoa kauli hiyo wakati
akizungumza na wazee wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa ‘Mshikamano
Saccos’, muda mfupi baada ya mzee Paschal Nyambibo (87) kumsihi agombee
nafasi hiyo mwaka 2015 kutokana...
SH. 500/- SASA ITAKUWA SARAFU BADALA YA NOTI ILI KUIFANYA ISICHAKAE HARAKA
KUTOKANA na kuchakaa haraka kwa noti ya shilingi 500 na kiwango chake
kudumu kwenye mzunguko kwa miezi sita tu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
imesema inatarajia kubadili noti hiyo na kuwa ya sarafu.Akizungumza
na gazeti la Tanzania Daima juzi kwenye viwanja vya maonesho ya
kimataifa ya biashara, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Fedha,
Abdul Dollah, alisema mabadiliko hayo yatafanyika hivi karibuni
na sarafu hiyo itadumu kwenye mzunguuko kwa zaidi ya miaka 20 huku ikiwa
na ubora wake.Dollah alitaja sababu
nyingine ya uchakavu huo ni kutokana na noti hiyo kushikwa na watu wengi
kwenye mzunguko huku baadhi yao wakishindwa...
"WIMBO WA MAJANGA UMENIPA DILI LA KUREKODI MOVIE AFRIKA KUSINI "– SNURA.
MWIGIZAJI wa kike na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Snura Mushi
amedai kuwa muziki ulimpa dili ya kwenda kurekodi filamu Afrika ya
Kusini...
Anasema kuwa dili hilo amelipata kutokana na kufanya vizuri katika muziki hasa nyimbo yake ya
Majanga.
“Filamu kwa sasa inachangamoto sana .Hilo lilinifanya nirudi katika
muziki huku nikichagua filamu za kuigiza na kujikita katika muziki zaidi
ambao unanifanya niwe bussy sana..
" Lakini ninachofurahia kupitia nyimbo
yangu ya majanga nilipoenda kuirekodia Afrika kusini Nnilipewa
uhusika mkuu kuigiza filamu ya Tandeka,”anasema Snura.
Snura anadai kuwa watayarishaji walimuona...
FBI WAINGIA ARUSHA KUCHUNGUZA BOMU LA SOWETO
Askari
wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), tayari wapo Arusha
kushirikiana na polisi ili kuchunguza tukio la mlipuko wa bomu la kutupa
kwa mkono kwenye mkutano wa kampeni za Chadema.
Katika
tukio hilo lililotokea Juni 15, mwaka huu Viwanja vya Soweto, eneo la
Kaloleni, Arusha, watu wanne walipoteza maisha huku zaidi ya 60
wakijeruhiwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Lebaratus Sabas, alithibitisha ushiriki wa FBI katika upelelezi huo.
Licha
ya FBI, polisi wanashirikiana na wenzao kutoka nchi jirani ya Kenya,
ambao wana uzoefu na matukio ya milipuko ya mabomu yanayotokea nchini
mwao mara kwa mara, hasa baada ya nchi...
BOMOA BOMOA YA POMBE MAGUFULI YAANZA.....JENGO LA BUSINESS PARK ( GREEN ACRES ) LABOMOLEWA
Baada
Waziri wa Ujenzi, Pombe Magufuli kutoa maagizo kwa wenye majengo yaliyo
pembezoni mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi, kubomoa wenyewe majengo
yao ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo, kuonekana yakisua sua,
hatimaye leo ameanza rasmi kazi ya kubomoa kwa Greda katika majengo ya
wale walioonekana kukaidi agizo hilo.
Katika kutekeleza agizo hilo zoezi
hilo limeanzia kwenye Jengo la Business Park (Green Acres) lililopo
eneo la Victoria ambapo hadi hivi sasa zoezi hilo bado linaendelea pande
hizo chini ya usimamizi ya Askari
Msongamano pande hizo.....
Tayari
ukuta ukiwa umeshashushwa...
No comments:
Post a Comment