Waziri wa Fedha, William Mgimwa,
amesisitiza uamuzi wa Serikali kuendelea kutoza Sh 1,000 kwa kila mwezi
kwa laini ya simu, licha ya kampuni za simu na wanasiasa kupinga.
Akizungumza
na mwandishi juzi, Mgimwa alikumbusha wanaolalamikia kodi hiyo, kwamba
suala la ulipaji kodi kwa taasisi au watu binafsi, ni la kisheria
kulingana na mapato yao na hali halisi iliyopo.
Pia alieleza
kushangazwa na matangazo ya baadhi ya kampuni kuhusu utozwaji kodi
wananchi akisema wananchi ndio wanataka barabara, maji na umeme vijijini
na kodi hizo zinakwenda kutumika huko.
Kwa mujibu wa Mgimwa, kodi
ya laini za simu na ya intaneti, imetengwa...
CHADEMA YAJITOA KUWANIA UMEYA WA ARUSHA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), kimeamua kuachana na kuwania umeya wa Jiji na badala yake
kimemwomba Meya, Gaudence Lyimo (CCM), atende haki.
Katibu wa
Kanda ya Kaskazini wa chama hicho, Amani Golugwa alisema jana, kwamba
Chadema haina uroho wa madaraka kama baadhi ya watu wanavyofikiri, bali
inasimamia vipaumbele vya maendeleo.
Hata hivyo, kauli hiyo
inapingana na nyingine ya chama hicho ya wiki hii pia, kwamba ushindi
katika uchaguzi mdogo wa kata nne, ni chachu katika msimamo wa chama
kutaka uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha, urudiwe.
Mwenyekiti wa
Madiwani wa Chadema, Isaya Doita, ndiye aliyenukuliwa wiki...
No comments:
Post a Comment