EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, June 18, 2013

HATIMAYE VAN KOCHA VILLA BOAS ATANGAZA RASMI KUTOTIMKA KTK KLABU YAKE YA SASA WAKATI KLABU ILIYOKUWA IKIMUWINDA PSG IKIMTANGAZA CAPELLO KUWA KOCHA WA KLABU HIYO HAPO JANA


IMEWEKWA JUNI 19, SAA 1:30 ASUBUHI 
KOCHA Andre Villas-Boas ameripotiwa kupiga chini ofa ya kuifundisha Paris Saint-Germain ili abaki Tottenham.
Mabingwa hao wa Ufaransa walitaka Mreno huyo arithi mikoba ya Carlo Ancelotti, anayeelekea Real Madrid, lakini sasa wamehamishia mawindo yao kwa Fabio Capello.
Inafahamika Villas-Boas alipewa ofa ya Mkataba wa miaka mitatu na mabilionea wa Qatari wanaoimiliki PSG baada ya majadiliano na wakala wake, Carlos Goncalves, lakini mwalimu huyo kijana wa miaka 35 anataka kufanya mambo adimu Spurs waliomchukua msimu uliopita baada ya kutupiwa virago Chelsea.
Staying put: Villas-Boas is reportedly looking to stay at White Hart Lane
Anabakit: Villas-Boas ameripotiwa kubaki White Hart Lane
Work to do: Villas-Boas will be looking to take Spurs up a notch after their fifth-place finish last season
Kazi ya kufanya: Villas-Boas anataka kuipaisha matawi ya juu zaidi Spurs kutoka nafasi ya tano aliyowapa msimu uliopita

Tottenham wanatarajiwa kubomoa benki kumpa fedha za kutosha Villas-Boas, aliyebakiza miaka miwili katika Mkataba wake White Hart Lane, ili kujenga kikosi cha nguvu cha kukata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.
Miongoni mwa wachezaji anaowataka ni kiungo wa Corinthians, Paulinho, wakati Spurs pia ni klabu pekee iliyoomba kumsajili kiungo wa Atletico Mineiro, Bernard. Wakala wake amesema: "Dortmund hawajawasilisha mapendekezo na Tottenham ni washindani pekee,".
Villas-Boas pia inaelezwa anavutiwa na ushindani wa kupambana na bosi wake wa zamani, Mreno mwenzake Jose Mourinho katika Ligi Kuu England msimu ujao.
Plan B: Russia boss Capello could be drafted in for a season
Mpango B: Kocha wa Urusi, Capello anaweza kuwa kazini msimu ujao

Taarifa za jana usiku nchini Ufaransa zinasema kocha wa zamani wa England, Capello atakuwa mwalimu mpya wa PSG kwa Mkataba wa mwaka mmoja.
Kocha wa zamani wa England, Capello anatazamiwa kuwa mpango B wa PSG, licha ya kwamba bado ana Mkataba wa mwaka mmoja Urusi.
Urusi ipo kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil,na kuna uwezekano Capello akarejea katika timu hiyo ya taifa baada ya msimu mmoja na PSG kukamilisha majukumu yake katika Kombe la Dunia.
Merry-go-round: Carlo Ancelotti looks to be on his way to Real Madrid
Carlo Ancelotti anatarajia kuhamia Real Madrid
Big season: PSG were French champions, and are looking to build an empire
Msimu mzuri: PSG walikuwa mabingwa Ufaransa na wanataka kujiimarisha zaidi

NANI ZAIDI KATI YA MEXICO NA MWENYEJI BRAZIL LEO KATIKA KOMBE LA MABARAA HIZI NI TAKWIMU ZA NCHI HIZI KATIKA HISTORIA YAO YA SOKA
Tuna masaa kadhaa ya kusubiri mechi ya pili wa kombe la mabara. Mchezo huo utakuwa dhidi ya Mexico na hizi ndio takwimu zinazohusisha mechi walizokutana magwiji hawa wa soka la bara la Amerika. 

 - Huu utakuwa mchezo wa nne kati ya Brazil-Mexico katika kombe la mabara, hivyo kuifanya mechi hii ndio ndio iliyochezwa mara nyingi zaidi katika historia ya michuano hii - mechi nyingine iliyochezwa mara nyingi ni Brazil-USA

 - Mchezo huu utakuwa wa 30 kwa Brazil katika michuano hii, ikiwa ndio timu iliyocheza mechi nyingi zaidi. 


 - Mexico wanawafuatia Brazil kwa kucheza mechi nyingi, mchezo wao wa leo utakuwa wa 21. 


 - Timu hizi mbili zimekutana mara 37, huku Seleção wakiongoza kwa ushindi wa mechi 21, wakati Mexico wameshinda mara 10.


 - Ushindi wa muhimu zaidi kwa Mexico katika hizo mara 10 ulikuwa mwaka 1999 katika kombe la mabara, ulikuwa mbele ya mashabiki wao 110,000 kwenye uwanja wa Azteca stadium


-  Mechi hii inazikutanisha timu pekee kwenye kombe la mabara 2013 ambazo zimeshashinda ubingwa wa kombe la mabara. 


 - Ushindi wa mwisho wa Mexico kwenye kombe la mabara ulikuwa siku kama ya leo - tarehe 19 June, 2005. Ni miaka 8 kamili. 

Tuesday, June 18, 2013

NIGERIA YABAKI KUWA TIMU PEKEE KUTOFUNGWA KWENYE KOMBE LA MABARA TANGU KUANZISHWA KWAKE BAADA YA KUIPA KIPIGO CHA 6-1 TAHITI

 Timu ya taifa ya Nigeria jana usiku iliitandika TAHITI mabao 6-1 kwenye michuano ya kombe la mabara inayoendelea huko nchini Brazil. Mchezo huo umetengeneza takwimu nyingi sana - zipo kama ifuatavyo:

- Nnamdi Oduamadi ndi mwanasoka wa kwanza wa kiafrika kufunga mabao 3 kwenye mechi moja katika michuano ya Mabara 

 - Jonathan Tehau ndio mchezaji wa kwanza wa Tahiti kwenye michuano ya FIFA 


 - Nigeria wanabaki kuwa ndio timu pekee ambayo haijawahi kupoteza mchezo katika historia michuano hii kwa timu ambazo zimewahi kushiriki. Wakishinda mara mbili na kutoa suluhu mara mbili. 


 - Jonathan Tehau ndio mchezaji wa kwanza kufunga kwa pande zote kwenye mechi ya michuano ya FIFA - na bado timuyake ikafungwa. Wachezaji sita wengine waliowahi kufanya hivyo wote timu zao walizokuwa wakizichezea zilishinda mechi zao. 


 - Matokeo ya Tahiti 1-6 Nigeria ni matokeo ya moja kati ya mechi 8 za kombe la mabara zilizozaa magoli mengi - 7.  Ni mechi moja tu ya Brazil 8-2 Saudi Arabia ndio imezidi idadi hiyo ya mabao kwa mechi. 

HUYU NDIO MCHEZAJI MWENYE UMRI MKUBWA ZAIDI KUWAHI KUCHEZA KWENYE KOMBE LA MABARA - ANATOKA AFRIKA

Siku kama ya leo 2005Golikipa wa Tunisia Ali Boumnijel alicheza kwenye mechi dhidi ya Ujerumani kwenye mashindano ya kombe la mabara akiwa na miaka 39 na miezi miwili, na akaweka rekodi ya mchezaji mwenye umri mkubwa kabisa kushiriki kwenye michuano hiyo.

SIKU KAMA YA LEO MWAKA 2009: EGYPT YAWEKA REKODI YA KUWA TIMU YA KWANZA KUIFUNGA ITALIA

Siku kama ya leo mwaka 2009Mechi kati ya Italy na Egypt ilikuwa ni ya 100 kuchezwa kwenye historia ya kombe la mabara. Egypt waliifunga Italia kwa 1-0, na hivyo kuwa timu ya kwanza kutoka Africa kuifunga Azzurri.

THIAGO ALCANTARA APIGA HAT TRICK NA KUIPA SPAIN UBINGWA WA EURO (U21) KWA USHINDI WA MABAO 4-2 DHIDI YA ITALIA


Spain vs Italy 4:2 GOALS HIGHLIGHTS (U21 EURO... by footballdaily1

SAKATA LA USAJILI WA CRISTIANO RONALDO - REAL MADRID WAPO TAYARI KUMLIPA FEDHA ANAYOTAKA - TATIZO LABAKI KWENYE HAKI ZA TASWIRA YAKE.

Cristiano Ronaldo anakaribia kukubaliana na Real Madrid juu ya mkataba mpya wa kuendelea kubaki Santiago Bernabeu - kwa klabu hiyo ya jiji la Madrid kumfanya Ronaldo kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi kuliko wote kwenye ulimwengu wa soka duniani.

Madrid wapo kwenye mazungumzo ya mwisho mwisho na wawakilishi wa Ronaldo kwa dili lenye thamani ya €155 million kwa mkataba wa miaka mitano - mkataba ambalo utamfanya Ronaldo aweke kibindoni €15m kwa mwaka baada ya kukatwa kodi - dili ambalo linatajwa kuwa la thamani zaidi katika historia ya soka duniani.

Ronaldo, ambaye amefunga mabao 201 katika 199 ndani ya misimu minne aliyokaa Santiago Bernabeu, aliwapa tumbo joto viongozi wa Madrid baada ya alhamisi ya wiki iliyopita kuandika kwenye mtandao wa Twitter kwamba: "All the news about my renewal with Real Madrid are false." 


Ronaldo ambaye miezi kadhaa huko nyuma aliwahi kukaririwa akisema hana furaha ndani ya Madrid katika kile alichosema kwamba ni sababu zinazomfanya asiwe na furaha ndani ya klabu hiyo viongozi wa Madrid wanazifahamu- sababu ambazo inasemekana zimetokana na sapoti ndogo anayopata kutoka kwa klabu yake hasa katika mbio za kugombea Ballon d'Or, pia kitu kingine ni ugomvi wake na mchezaji mwenzie  Marcelo.

Madrid walimsajili Ronaldo kutoka Manchester United kwa rekodi ya uhamisho ya €94 million wakati wa kiangazi mnamo mwaka 2009, mara tu baada ya kurudi kwenye uongozi kwa Raisi  Florentino Perez. Kwa sasa Ronaldo analipwa kiasi cha €10m baada ya kodi.

Wakati Ronaldo aalipowasili Spain, kulikuwa na kitu kinachoitwa 'Beckham Law', ambayo iliwaruhusu wageni ambao wameishi nchini humo kwa miaka chini ya 10 na ambao wanavuna zaidi ya kiasi cha €120,000  kwa mwaka kulipa kodi ya chini kiasi cha asilimia 23 na sio ile ya kawaida ya asilimia 45, bado ilikuwepo. David Beckham alikuwa mmoja wa watu wa kwanza  kupata faida ya sheria hiyo baada ya kuhamia Madrid akitokea kupata  Manchester United mnamo mwaka 2003.

Japokuwa baadae serikali ya Spain ikaifuta sheria hiyo na sasa mkataba mpya wa Ronaldo utakuwa unakatwa kiasi cha 52% kama kodi. Hivyo, Madrid itabidi watoe package ya €31m ili baada ya makato Ronaldo abaki na kiasi cha €15m ambacho anakitaka.

Madrid, wanatambua umuhimu wa kuendelea kuwa na Ronaldo. Klabu hiyo hivi karibuni imemkosa Neymar, wakati wakionekana kukata tamaa ya uwapata wachezaji wa Dortmund Ilkay Gundogan na Robert Lewandowski. Wachezaji wengine ambao walikuwa kwenye hesabu zao kama vile Sergio Aguero na Radamel Falcao, hawatoenda Madrid pia, wakati Gareth Bale ni gharama zaidi kumpata na hataki kuomba uhamisho kutoka Tottenham na huku Edinson Cavani anaonekana kuwa hana thamani ya fedha ambayo Napoli wanaitaka kutokana mauzo ya Cavani. Hivyo kubaki na Ronaldo ni jambo muhimu.

Raisi wa klabu hiyo alikaririwa hivi karibuni akisema kwamba atafanya chochote kuhakikisha Mreno huyo anabakia ndani ya jiji la Madrid hata kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi kwenye ulimwengu wa soka.

Madrid sasa wapo tayari kumpa Ronaldo anachokitaka na kumfanya apate fedha nyingi kuliko Lionel Messi, ambaye analipwa kiasi cha €13m kwa mwaka kabla ya bonasi ndani ya Barcelona, na Falcao, ambaye anapata kiasi cha €14m kwa mwaka ndani ya Monaco. Samuel Eto'o analipwa kiasi cha €20m kwa mwaka na Anzhi Makhachkala, ingawa dili hilo la mcameroon huyo lina muda wa miaka mitatu tu na kwa ujumla dili la Ronaldo litampita Eto'o.

Tatizo kubwa na kizingiti kikubwa katika makubaliano ya mkataba mpya wa Ronaldo na Madrid ni suala la haki za taswira yake. Cristiano kwa sasa anamiliki asilimia 60 wakati klabu inachukua 40 zinazobakia. Ronaldo anahitaji maboresho makubwa kwenye suala hili - inaaminika anataka haki zake zote za taswira yake kwa maana ya asilimia 100 - kitu ambacho Madrid hawakubaliani nacho. Hapo ndipo makubaliano juu ya mkataba mpya yanapochelewa.

TIMU YA THAILAND YASAKA WACHEZAJI TANZANIA - GOSAGE MTUMWA APEWA ITC KWENDA KUCHEZA YEMENI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Mtanzania Gossage Mtumwa ili aweze kucheza mpira nchini Yemen.

Mtumwa ambaye anatoka katika kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji cha Rollingstone cha Arusha aliombewa hati hiyo na Chama cha Mpira wa Miguu cha Yemen (YFA) kwa ajili ya kucheza nchini humo.

TFF inamtakia kila la kheri Mtumwa katika safari yake ya Yemen, na ni matarajio yetu kuwa atakuwa balozi mzuri wa Tanzania nchini humo ili wachezaji wengine wa Tanzania nao wapate fursa ya kucheza mpira wa miguu nchini Yemen.

KLABU THAILAND YASAKA WACHEZAJI TANZANIA
Klabu ya Thai Port Football ya Thailand inatafuta wachezaji nchini Tanzania kwa ajili ya kucheza mpira wa miguu nchini humo na katika nchi nyingine barani Ulaya.

Kupitia kwa wakala wake, klabu hiyo imetuma taarifa kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikitaka wachezaji wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 28 kwa ajili ya kuwafanyia majaribio ambapo watakaofuzu watacheza nchini humo na katika klabu nyingine za Ulaya ambazo wana ushirikiano nazo.

Wachezaji wenye nia ya kufanya majaribio wanatakiwa kutuma taarifa za wasifu wao (CV) kwa klabu hiyo kwa njia ya emaili, wawe na pasi ya kusafiria pamoja na pasi ya mchezaji (player passport).

Wakala atapitia vitu hivyo, na kwa wachezaji atakaowahitaji atawatumia tiketi za ndege na viza kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio nchini humo, na watakaofanikiwa kabla ya kusaini nao mikataba watawasiliana na klabu zao nchini (kwa wale wenye klabu).

NSAJIGWA, BEN MWALALA NA WACHEZAJI WENGINE KUMALIZA KOZI YA UKOCHA JUMANNE

Nahodha wa zamani wa Yanga Shedrack Nsajigwa akiwa na Baadhi ya makocha wakiwemo wachezaji wa zamani wakifuatilia mafunzo ya ukocha ngazi ya pili.

Kocha mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage akitoa somo kwa makocha wanashiriki kozi ya ukocha ngazi ya pili ndani ya darasa kwenye Ukumbi wa Harbours Club, Kurasini.

Kocha mkuu wa Twiga Stars akitoa somo kwa makocha wa kozi ya ngazi ya pili kwa vitendo
KOZI ya makocha wa ngazi ya pili (Intermediate) inayosimamiwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), inatarajiwa kufungwa Jumanne ijayo baada ya kudumu kwa wiki nne.
Kozi hiyo ilianza Juni 3 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Harbours Club, uliopo Kurasini chini ya Mkufunzi Rogasin Kaijage, ambaye ni Kocha wa timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ ambapo makocha mbalimbali pamoja na wachezaji wa zamani wamejitokeza kushiriki.
Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo alisema kozi hiyo imekuwa na mafanikio na wanatarajia makocha walioshiriki katika kozi hiyo watakuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza mpira wa miguu katika mkoa wa Dar es Salaan na Taifa kwa ujumla.
“Hadi sasa tunashukuru kuona tunafanikisha kozi hii ambayo wengi wameitikia wito, mwisho wa kozi hii ndio mwanzo wa kozi nyingine.
“Lakini haya ya kozi ya makocha ni moja ya majukumu ya Kamati ya Ufundi ya DRFA yaliyoainishwa katika Katiba, hivyo hili ni moja ya shabaha yetu na mengine mengi mazuri yanafuata,” alisema Mharizo.
 Kozi hiyo ni ya kwanza kuendeshwa na DRFA tangu kuingia madarakani kwa uongozi mpya wa chama hicho Desemba 12, chini ya Mwenyekiti wake Almas Kassongo.

SUNDERLAND NA SYMBION KUJENGA ACADEMY MBILI ZA SOKA DAR ES SALAAM


CEO wa klabu ya Sunderland, Margaret Byrne, ameusifia ushirikiano na Tanzania kwamba ni hatua kubwa kuendelea mbele.
The Black Cats wameingia mkataba na kampuni ya nishati ya Power kujenga cademy kubwa ya soka nchini, ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Raisi Jakaya Kikwete alitembelea makao makuu ya klabu ya Sunderland huko Wearside siku ya jumapili katika kukata rasmi utepe wa kuanza kwa project hiyo.
“Ni siku muhimu kwa klabu na klabu na mji wetu,” Byrne alisema.
“Kutembelewa na mheshimiwa Raisi hapa wakati akiwa UK kuhudhuria mkutano wa viongozi wa G8 ni jambo kubwa kutoka kwake na mawaziri wake. Ni zuri sana kwetu.
Hatua za mwanzo kwa ajili ya Academy zilizinduliwa siku hiyo ya jumapili, kwenye tukio ambalo lilihudhuriwa na mwenyekiti wa Sunderland Ellis Short.
Project hiyo itaisaidia Tanzania katika kukuza soka lake pia kuwapa nafasi kubwa vijana wadogo kabisa kuweza kuendeleza vipaji vyao kwenye academy hiyo. 
Sunderland watajenga majengo pamoja na kutoa makocha wa kufundisha.
“Hatua ya kwanza itatuhusisha sisi kufanya kazi na Symbion Power kujenga academy ya kijamii, tukiruhusu watoto wengi kuja na kufurahia kucheza mchezo wa soka,” Byrne alielezea.
“Hatua ya pili itatuhusisha sisi kufanya kazi na Symbion labda ikiwezekana na taasisi nyingine kujenga kituo cha kisasa cha kufundishia soka.
“Tutoa usaidizi mkubwa wa vifaa vingi tunavyotumia kwenye academy yetu ya Academy of Light na pia na maarifa tuliyoyapata na tunayoyapata kutoka kwenye project ya EPPP (Elite Player Performance Plan).

No comments:

Post a Comment