EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, February 25, 2014

GALATASARAY v CHELSEA: SNEIJDER ADAI MOURINHO ANATUJUA, TUNAMJUA!


SNEIJDERWesley Sneijder anaamini wanamjua nje ndani Jose Mourinho na hilo litaisaidia Timu yao Galatasaray kuibwaga Chelsea watakapokutana Jumatano Usiku ndani ya Türk Telekom Arena Ali Sami Yen Spor Kompleksi huko Istanbul, Uturuki kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Sneijder, Mchezaji wa Kimataifa wa Holland, alikuwemo kwenye Kikosi cha Inter Milan Mwaka 2010 chini ya Jose Mourinho kilichotwaa Trebo, ikiwemo UCL.
Sneijder anaamini uzoefu wake chini ya Mourinho utaisaidia Galatasaray kuibwaga Chelsea.
Mchezaji mwingine wa Galatasaray aliewahi kuwa na Jose Mourinho ni Didier DrogbaMANCINI_N_DROGBAambae alinunuliwa na Mourinho Mwaka 2004 kutoka Marseille na kukaa Klabu hiyo hadi Mwaka 2012 ambako kwenye Mechi yake ya mwisho alifunga Penati ya mwisho ya Mikwaju ya Penati 5 walipoibwaga Bayern Munich kwenye Fainali ya UCL na kutwaa Ubingwa wa Ulaya Mjini Munich.
Sneijder amedai yeye na Drogba watamsaidia Kocha Roberto Mancini, aliewahi kuwa Manchester City, kuandaa Timu kwa ajili ya Mechi na Chelsea.
Amesema: “Mourinho anatujua vizuri na hilo ni udhaifu kwetu lakini hilo pia linatusaidia sisi kwani tunamjua Mourinho vizuri sana, pengine tunamjua vyema zaidi kupita Wachezaji wa Chelsea wanavyomjua!”
Aliongeza: “Chelsea ni Kikosi bora, kila Mtu lazima akubali, lakini tukionyesha ari ile ile tuliyowatoa Juventus, tunaweza kupata matokeo mengine makubwa!”
Nae Selcuk Inan, Kiungo wa Galatasaray, vile vile anaamini Türk Telekom Arena Ali Sami Yen Spor Kompleksi inatisha kwa Timu ngeni hasa toka kwa Mashabiki wao wenye vimbwanga kupindukia.
Amesema: “Jinsi Mashabiki wanavyotushangilia ni kitu kikubwa. Wao ni kama Mchezaji wetu wa 12!”

No comments:

Post a Comment