EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, January 16, 2014

MOURINHO AFURAHIA KUMNASA MATIC TENA.


MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amekiri kufurahishwa na kumsajili kwa mara nyingine Nemanja Matic na kumsifia kuwa mmoja wa viungo bora kabisa hivi sasa. Nyota huyo wa kimataifa wa Serbia aliondoka Chelsea na kuhamia Benfica mwaka 2011 ikiwa kama sehemu ya Chelsea kumsajili David Luiz lakini kiungo huyo amerejea tena darajani kwa ada ya euro milioni 25. Ujio wa kiungo huyo umekuwa faraja kwa Mourinho ambaye amedai kuwa atakuwa sehemu muhimu katika kikosi chake ambacho kinafuukuzia taji la Ligi Kuu na Ulaya. Matic amerudi Chelsea kuchuana kutafuta namba katika kikosi cha kwanza na kina John Obi Mikael, Frank Lampard, Ramires na Michael Essien na ana uhakika kuwa safari hii anaweza kupata namba katika kikosi hicho.

No comments:

Post a Comment