MENEJA
LEKENDARI Sir Alex Ferguson anadhani Manchester City ndio wenye nafasi
kubwa kutwaa Ubingwa wa England Msimu huu huku akiwa kimya kuhusu nafasi
ya Kikosi cha Chelsea chini ya Meneja wao Antonio Conte.
Sir
Alex Ferguson, mwenye Miaka 74, aliongea hayo akiwa huko Nurenberg,
Germany alikokwenda kupokea Tuzo ya Walther Bensemann ambayo hutunukiwa
Watu waliotoa Utumisha Uliotukuka kwenye Soka.
Tuzo
hiyo hutolewa kwa ajili ya Kumbukumbu ya Bensemann ambae ndie
anasemekana ni Muasisi wa Soka la Germany ambae alianzisha Jarida la
Michezo, Kicker, Mwaka 1920.
Baadhi
ya Washindi waliopita waliowahi kutwaa Tuzo hii ni pamoja na Franz
Beckenbauer, Alfredo di Stefano and Sir Bobby Charlton.
Akiongea
na Jarida la Kicker, Sir Alex Ferguson, ambae alistaafu Umeneja Man
United Mwaka 2013 baada ya kuiongoza kwa mafanikio makubwa kwa Miaka 26
akitwaa Makombe 38, amezitaja Timu 5 zenye nafasi nzuri za kuwa Mabingwa
wa EPL, Ligi Kuu England.
Ferguson
alisema: “Nadhani wapo Wagombea Watano. Man City wao ndio wana nafasi
kubwa, Tottenham na Liverpool pia, lakini Man United pia wamo ikiwa
tutapata mtiririko mzuri hivi karibuni.”
Aliongeza: “Hata kama unalegalega nyuma kwa Pointi 6 au 8 bado inawezekana kuzikamata Timu 2 au 3!”
“Ushindani
na uzoefu kati ya Guardiola na Mourinho utaleta upinzani mzuri wa
kuvutia. Msiisahau Arsenal. Timu imeimarika sasa. Wamekuwa bora na
wakali. Nimefurahishwa sana na Chipukizi wao Alex Iwobi!”
Pia
Ferguson anaamini ufundi wa Bosi wa Manchester City Pep Guardiola
hauwezi kujadiliwa licha ya sasa kwenda Mechi 6 bila ushindi.
Vilevile, Ferguson alimsifia Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino, na kumsema ana uwezo mkubwa.
Alisema:
“Mauricio Pochettino anao uwezo na Spurs ina mchanganyiko mzuri wa
Vijana na wale Wazoefu. Wachezaji wao wakubwa, Harry Kane na Eric Dier,
ni majeruhi lakini bado wapo nafasi nzuri!”
Mbali
ya kudai kuwa Meneja wa Chelsea Antonio Conte ameirejesha Chelsea juu
wanapostahili, Ferguson hakueleza lolote kuhusu nafasi ya Chelsea Msimu
huu.
EPL - LIGI KUU ENGLAND
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 29
1430 Sunderland v Arsenal
1700 Man United v Burnley
1700 Middlesbrough v Bournemouth
1700 Tottenham v Leicester
1700 Watford v Hull
1700 West Brom v Man City
1930 Crystal Palace v Liverpool
Jumapili Oktoba 30
1630 Everton v West Ham
1900 Southampton v Chelsea
Jumatatu Oktoba 31
2300 Stoke v Swansea
No comments:
Post a Comment