EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, October 31, 2013

ABOUD:MASHAMBULIZI YA TINDIKALI ZANZIBAR NI UTEKELEZAJI WA MIPANGO YA KISIASA



Serikali Visiwani Zanzibar, imesema kuwa mashambulizi ya kutumia tindikali dhidi ya viongozi wa dini na Serikali visiwani humo, ni utekelezaji wa mipango ya kisiasa na si sehemu ya chuki za kidini.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake eneo la Vugha, Zanzibar, ambapo amesema wanaotekeleza mashambulizi hayo, ni watu waovu wenye nia ya kuleta vurugu na kuivunja nchi katika vipande, na tayari katika hii wanaelekea kufanikiwa kwa kuitia doa Serikali ya Umoja wa Kitaifa visiwani humo.

 Amesema mashambulizi hayo yameleta taswira mbaya kwa Wazanzibari wenyewe na Tanzania kama nchi, kwani yanailenga jamii moja ambayo siku jamii hiyo ikiishiwa uvumilivu, taifa linaweza kuingia katika machafuko na kuathiri kwa kiasi kikubwa amani, mshikamano wa kitaifa na utulivu visiwani humo.Waziri huyo ameonya iwapo Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar utavunjika, basi wanaotoka visiwani hawatabaki salama kama Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alivyowahi kuonya siku za nyumaWaziri Mohammed amebainisha kuwa, faida za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni nyingi kuliko kero zinazolalamikiwa, huku akitaja faida hizo kuwa ni pamoja na fursa ya kumiliki ardhi, soko la watu milioni 40 la bara, kuishi na kufanya kazi upande wowote.

No comments:

Post a Comment