NA MSHAM NGOJWIKE
TIMU ya soka ya shule ya
Sekondari Mlalo Day (Mlalo Stars), ya Wilayani Lushoto imedhamiria kutetea
ubingwa wao wa michuano ya Shambalai Cup inayoendelea katika jimbo hilo la
Mlalo.
Akizungumza na SWACO jana
kutoka Lushoto,mwalimu wa michezo wa shule hiyo,Fineas Mashombela alisema
kwamba ameiandaa timu yake kikamilifi kuhakikisha ubingwa unatua mikononi mwao
tena.
“Ligi imeshaanza lakini sisi
bado hatujaanza kucheza kwani ndio mabingwa watetezi tunasubiri mpaka raundi ya
pili,kwa ujumla nimekiandaa kikosi changu kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu,”
alisema.
Alisema moja ya mambo
anayoyafanyia kazi ni safu yake ya ushambuliaji ili kufunga mabao mengi zaidi
kuliko msimu uliomalizika na pia safu yake ya ulinzi isiruhusu mabao ya
kizembe.
“Kwa sasa kitu ambacho
ninakifanya ni kuisuka safu yangu ya ushambuliaji ili kupata mabao mengi zaidi
na pia safu ya ulinzi isije ikaruhusu mabao ya kizembe,kwa ujumla naamini
hakuna kitakachoharibika,” alisema.
No comments:
Post a Comment