Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani,Thomas Mihayo.
Pia amewataka kutambua kwamba wametumwa Dodoma na wananchi kuwapatia Watanzania Katiba bora na si kutimiza matakwa ya watu wachache.
Alitoa rai hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kusambaza uelewa wa rasimu ya Katiba kwa wananchi inayotambukila kama “Big Bang Constitutional Campaign (BBCC) iliyoandaliwa na asasi za kiaraia (Azaki) na kuratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Alisema mchakato wa Katiba si wa wanasiasa, wanasheria wala wasomi pekee, bali ni wa wananchi wote, hivyo wanapaswa kushirikishwa katika kila hatua.
“Ikiwa Katiba inayopendekezwa itakuwa bora, basi wananchi watakuwa na shauku ya kushiriki kikamilifu katika kura ya maoni ili kujipatia Katiba inayofaa na si vinginevyo.
Tunatambua kuwa katika kipindi hiki cha mpito, kila kundi na kila kiongozi atawajibika kwa mwenendo, kauli au matendo kuhimiza chuki, fujo, vurugu au uvunjifu wa amani kwa njia yoyote” alisema.
Pia Jaji Mihayo alitoa wito kwa viongozi wa dini na vyama vya siasa kuhimiza wafuasi wao kujali zaidi maslahi ya taifa kuliko maslahi mengine.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment