TIMU ya soka Villa Squad ya Magomeni, juzi
ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Juhudi Fc ya Mabibo katika mechi ya
kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa shule ya msingi Makurumla Mwembechai.
Juhudi ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 10 kwenye kipindi
cha kwanza cha mchezo huo kupitia mshambuliaji wake Salgado Kipara na kuzifanya
timu hizo kwenda mapumziko Juhudi wakiwa mbele kwa bao hilo.
Kipindi cha pili timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu kila moja
ikikosa nafasi za wazi kutokana na washambuliaji wa pande zote kukosa umakini
wa umaliziaji.
Dakika ya 79 Omari Mohamed alifanikiwa kuisawazishia timu yake ya Villa
Squad bao baada ya kuwatoka mabeki wa timu pinzani na kuachia shuti kali
lililojaa wavuni moja kwa moja.
Baada ya mchezo huo kumalizika kocha mkuu wa Juhudi FC,Kaduguda Reuben
alisema kuwa timu yake ilicheza vizuri ila hawakuwa na bahati ya kuibuka na
ushindi.
“Wachezaji wangu walijitahidi kucheza vizuri kwa dakika zote 90 ila bahati
haikuwa upande wetu,mwamuzi alichezesha vizuri sana ndio mana hapakuwa na
malalamiko kutoka kwa pande zote,” alisema.
No comments:
Post a Comment