MBAO FC YAWATISHA YANGA WASEMA WAO SI WAMCHEZOMCHEZO
Wakati
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ikiendelea leo Ijumaa Oktoba
28, 2016 kwa mchezo mmoja, kwa siku ya kesho Jumamosi Oktoba 29, mwaka
huu kutakuwa na michezo mitano wakati kwa siku ya Jumapili kutakuwa na
michezo miwili ya raundi ya 13, ligi ikielekea ukiongoni mwa mzunguko wa
kwanza.
kesho itakuwa ni zamu ya Toto Africans
ya Mwanza dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
na Mbeya City ya Mbeya itakayokuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea
kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mwadui ya Shinyanga inatarajiwa
kuialika Simba kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga wakati
African Lyon ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons ya
Mbeya kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ilihali JKT Ruvu na Ndanda
zitachuana Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili
Oktoba 30, 2016 Young Africans itacheza na Mbao FC kwenye Uwanja wa
Uhuru huku Ruvu Shooting ikiwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa
Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment