EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, December 5, 2013

ULIMWENGU APATA OFA KIBAO ULAYA, ASEMA KIKIELEWEKA ANAONDOKA MAZEMBE

http://thomasulimwengu.files.wordpress.com/2013/09/1-tu-11.jpg
Thomasi Ulimwengu
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu amesema kwamba ndoto za kuhamia Ulaya zinakaribia kutimia, kwani ana ofa nyingi kutoka nchi mbalimbali, zikiwemo Hispania, Ufaransa, Ubelgiji na Italia.

Akizungumza Kutoka nchini kenya , Ulimwengu aliye kwenye kikosi cha Bara, Kilimanjaro Stars kinachoshirki Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge amesema kwamba ana matumaini makubwa ya kuhamia Ulaya.

“Nina ofa nyingi na zinafanyiwa kazi kwa sasa, nadhani muda si mrefu nitaondoka Afrika, tuombe Mungu,”alisema mshambuliaji huyo wa Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 
  Ulimwengu anacheza klabu moja na Mtanzania, mwenzake Mbwana Ally Samatta, TP Mazembe na wote kwa sasa ndiyo wachezaji wakubwa zaidi na tegemeo wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment