EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, December 5, 2013

BREAKING NEWS;NELSON MANDELA AAGA DUNIA

Pumzika kwa amani baba wa Taifa
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amesema usiku huu kwamba 'baba wa Taifa' la Afrika Kusini amefariki akiwa na umri wa miaka 95.
"Taifa letu limepoteza mtoto wake mkubwa. Watu wetu wamepoteza baba",".
Pumzika kwa amani shujaa;  Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amethibitisha Nelson Mandela amefariki akiwa na umri wa miaka 95
Nation's greatest son: Nelson Mandela lifts the World Cup trophy in Zurich, Switzerland, after FIFA's executive committee announced that South Africa would host the 2010 World Cup soccer tournament. South Africa's 'Greatest Son' died Thursday at 95
Mtoto mkubwa wa taifa: Nelson Mandela akiwa ameinua Kombe la Dunia mjini Zurich, Uswisi, baada ya Kamati ya Utendaji ya FIFA kutangaza Afrika Kusini itaandaa Fainali za Kombe la Dunia za 2010.


Nelson Rolihlahla Mandela alizaliwa Julai 18, mwaka 1918 na ndiye rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini. 
Alikuwa mwanasheria na mwanachama wa ANC aliyepinga siasa ya ubaguzi wa rangi Apartheid katika Afrika Kusini. 

  Mandela alitumikia kifungo cha maisha kwa miaka 27 kutokana na harakati zake za kuupinga ubaguzi wa rangi.

Alifungwa katika kisiwa cha Robben. Baada ya kuachiwa huru mwaka 1990 alianzisha sera ya maridhiano. Mwaka wa 1993, pamoja na Frederik Willem de Klerk alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani.

No comments:

Post a Comment